The House of Favourite Newspapers

Wadukuzi wa Bomba la Mafuta Walipwa Mabilioni

0

KAMPUNI ya Colonial ambayo inamiliki Bomba kubwa la mafuta nchini Marekani limeripotiwa kuwalipa wahalifu wa mtandaoni wanaofahamika kama DarkSide kiasi cha dola milioni tano $5m (£3.6m) kama kikombozi ,baada ya bomba hilo kuvamiwa mtandaoni.

 

Hali imekuwa tete kwa kampuni hiyo ya kusambaza mafuta ambayo imekuwa linapata wakati mgumu kufanya shughuli zake baada ya kudukuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha kuzimwa kwa huduma za mtandaoni katika bomba hilo kwa muda wa siku tano na hivyo kufanya usambazaji wa mafuta kuwa mgumu katika maeneo yote Marekani.

 

Siku ya Ijumaa, wateja wa teknolojia kubwa ya Japan ya Toshiba walisema upande wa ulaya nchini Ufaransa ulikuwa umeshambuliwa na genge hilo hilo la wahalifu wa mtandaoni .

 

Colonial imetangaza kurudisha operesheni zake siku ya Jumatano lakini ilitoa angalizo kuwa itachukua siku kadhaa kuanza kusambaza bidhaa na kurudi katika taratibu zake za kawaida.

 

Usitishwaji wa usamazaji wa mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya ndege katika taifa zima la Marekani kumesababisha bei za bidhaa hizo kupanda na sheria ya dharura kupitishwa Jumatatu ya kutangaza hali ya dharura.

 

Bomba hilo kwa kina la Colonial linabeba mapipa milioni 2.5 kila siku – sawa na 45% ya mahitaji ya mafuta ya Pwani ya Mashariki nchi hiyo na liinasambaza mafuta ya dizeli, ya petroli na mafuta ya ndege.

Leave A Reply