The House of Favourite Newspapers

Waendesha Baiskeli wa Ziara ya Twende Butiama 2024 Wachangiwa Mil. 70

0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ziara ya waendesha baiskeli kuelekea Butiama 2024, ambayo inadhaminiwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic.
Uzinduzi huu ulifanyika kama maendesho ya baiskeli ya kijamii “Pedal for Purpose,” ambayo ni mwanzo wa ziara hii kuelekea Butiama. Benki ya Stanbic imechangia kiasi cha shilingi milioni 70, ambazo zitatumika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa madawati 1,500, sekta ya afya kwa kuanzisha kliniki zinazozunguka kuhudumia mikoa mbalimbali, na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti 50,000.
Kiujumla ziara hii inategemea kuboresha Maisha ya watanzania 100,000. Kilele cha ziara hiyo kitafanyika Butiama, mkoani Mara, tarehe 14 Oktoba.

Mchezaji wa zamani toka Nigeria, Nwankwo Kanu (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi  Vodacom Twende Butiama 2024 uliofanyika jijini Dar es salaam.

Nwanko Kanu (kulia) mwenye baiskeli. Katikati ni CEO wa Stanbic Bank Tanzania, Manzi Rwegasira na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Philip Besiimire kwenye uzinduzi wa ziara hiyo.

Kutoka kushoto ni Nwanko Kanu, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Philip Besiimire na CEO wa Stanbic Bank Tanzania, Manzi Rwegasira.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Philip Besiimire (kushoto). Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira.
Leave A Reply