


RAIA wa Ethiopia zaidi ya kumi leo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakidaiwa kuwa wahamiaji haramu.
Awali watu hao walifikishwa mahakamani hapo na magari ya Idara ya Uhamiaji ambapo haikufahamika walikamatwa maeneo gani hapa nchini. Lakini habari za kuaminika ni kwamba walikamatwa wakiwa njiani hapa nchini wakiwa hawana hati za kuwaruhusu kuwapo nchini ambapo inaaminika walikuwa wanakwenda Afrika Kusini.
NA DENIS MTIMA/GPL

