
Mapambano ya usawa wa jinsia yanaendelea licha ya kwamba katika miaka ya karibumi kumekuwa na muamko mkubwa katika masuala ya usawa wa kijinsia hususani kwenye fursa mbalimbali ambazo wanawake wanapatiwa. Hata hivyo, bado safari ya inaendelea.
Mabinti wengi huanza safari ya maisha yao huku wakiwa na ndoto kubwa, lakini mara nyingi utamaduni wa makabila mengi hutamatisha ndoto hizi za wanawake na kufuta matumaini ya kusonga mbele na kuwabakisha kuwa na majukumu ya mama wa nyumbani. Kwa hivyo, hii inaondoa imani ya mabinti wengi ambao sasa mwisho wa siku wanaishi bila kujua thamani yao kwa jamii.
Leo, mitazamo inabadilika, na jinsia haionekani kama kikwazo kama ilivyokuwa zamani, kuzuia wanawake kutekeleza ndoto zao.
Josephine Kimambo na Shadya Jamali ni miongoni mwa wanawake wachache katika tasnia ya madini, wanaounda sehemu ya Idara ya Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo ya Geita Gold Mining Limited. Wote wawili wanaishi maisha ya kawaida katika ulimwengu uliojaa changamoto mbalimbali za usawa wa kijinsia.
”Kuamini kwamba kila mtu ni wa kipekee na anaweza kuacha urithi imethibitisha kutoka kwa mtazamo wao kwamba jinsia sio kikwazo maadamu wanajua kusudi la kuishi kwao.

Josephine Kimambo, ambaye sasa ni Afisa Mwandamizi, alijiunga na GGML mnamo mwaka 2012 kama mwanafunzi aliyehitimu chini ya mpango wa kuajiri wahitimu wa shahada ya kwanza. Baada ya kumaliza kufanikisha programu hiyo mnamo 2014, Josephine alipata ajira na kuchukua jukumu la Afisa wa udhibiti wa taka na kemikali na anafurahia jukumu lake ndani ya GGML hadi leo.
Josephine anaamini kuwa kila mtu ni mwandishi wa hadithi yake na ana uwezo wa kuifanya hadithi hii kuwa chanya au hasi. Kila mtu anaamua ikiwa atakaa kwa kuwa wa kawaida au la.
Vivyo hivyo, anaelezea, “Mtu yeyote anaweza kuwa wa kufanya makubwa zaidi maadamu amejitolea kujiendeleza na maendeleo ya kibinafsi.”
“Kufanya kazi katika sekta ya madini kama mwanamke sio ngumu kama inavyofikiriwa. Ni mazingira mazuri ya kufanyia kazi; hii ni kwa sababu kampuni inazingatia viwango vya kimataifa na wataalam ambao wanaendelea kuongeza maarifa yetu.
Kuna fursa nyingi za kukua kitaaluma iwapo mtu ataamua kuzingatia kufanya kazi kwa juhudi zake zote. Ninahimiza wanawake wengine wanaofanya kazi GGML na wale ambao wanataka kujiunga na tasnia ya madini kukataa kuwa wa kawaida na kujiepusha kutoa visingizio juu ya wao ni nani. Baada ya yote, kuwa mwanamkee sio sababu ya kukufanya ufeli,” anawasihi wanawake wengine.
Mfanyakazi mwenzi Josephine katika Idara ya HSE & T, Shadya Jamali anawahimiza wanawake kupuuza dhana zilizowekwa vibaya za kufanya kazi katika tasnia ya madini na kuondoa mashaka yoyote ya kibinafsi ili kufanikiwa kurejesha imani kwa wanawakee kufanya kazi katika tasnia hiyo.
“Kwa wanawake wangu wapenzi ambao wamekosa imani ya kufanya kazi hizi kutokana na dhana mbalimbali, tafadhali usiruhusu hofu ikuzuie kwa sababu kikwazo kikubwa maishani ni hofu. Kama mwanamke anayefanya kazi katika uwanja unaotawaliwa na wanaume, ninaelewa jinsi mazingira yanavyoweza kuwa magumu tunapokutana na vizuizi vingi, lakini hatupaswi kukubali kushindwa kwa urahisi.

Wanawake wana majukumu kadhaa ya kuleta mabadiliko katika maeneo yao na tunapaswa kuondoa imani zilizopitwa na wakati kwamba wanawake ni mama tu na sio wafanyakazi. Wanawake wanaweza kufanya yote mawili na hata zaidi kuliko wenzao wa kiume,” anasisitiza Shadya.
Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kama kampuni nyingine zinazotoa kipaumbele kudumisha mazoea bora katika mtaji wa watu.
Kampuni ina sera kali zisizo za ubaguzi na inathamini utofauti wa wafanyikazi wake ambao unaiwezesha kuwekeza kikamilifu katika mipango ambayo inakuza wanawake mahali pa kazi.
Moja ya mipango hii na GGML inadhamini wafanyakazi wake wa kike kushiriki katika Programu ya Wanawake viongozi wa baadaye inayosimamiwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Ni progamu ambayo inawaandaa kuchukua majukumu ya uongozi ndani na nje ya Kampuni.
NA MWANDISHI WETU

