The House of Favourite Newspapers

Wafahamu wadudu wenye protini zaidi samaki, kuku!

 

WANASAYANSI katika mojawapo wa vyuo vikuu nchini Kenya wako kwenye harakati za kuwashauri watu wale wadudu. Ni miaka kumi na miwili tangu chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Kenyatta kuanza mradi wa wadudu.

 

Mradi huo umeyavutia mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia, Shirika la Chakula Ulimwenguni (WHO) ambayo yanaamini kuwa kilimo cha wadudu ni dawa nzuri ya kukabliana na uhaba wa chakula.

 

WHO  linabashiri ongezeko la mahitaji ya chakula, huku vipande vya ardhi vikiendelea kudidimia ifikapo mwaka 2050.

 

Inakadiriwa kwamba ifikiapo mwaka huo idadi ya watu ulimwenguni itakuwa imeongezeka hadi watu bilioni 10. Wanasayansi sasa wanatarajia kuwa wadudu hawa wadogo wenye virutubisho watachangia kuziba mwanya wa uhaba wa chakula.

 

Wanasema kuwa wadudu hao wana protini zaidi ya mara tatu ukilinganisha na nyama ya ng’ombe, mara mbili zaidi ya samaki na kuku.  Prof Kinyuru anasema kuwa chuo hicho kinamiliki yamkini wadudu milioni mbili.

 

”Hebu tafakari, nafasi ya ng’ombe milioni mbili, kuku milioni mbili, ni eneo la bunge lote.  Hakika protini hii nzuri ina madini ambayo mwili wako unahitaji. Kuna madini ambayo huwezi ukapata kwenye samaki ama kuku.

 

 

Kwa kipindi cha miezi mitatu senene huwa wako tayari kuliwa. Wao huanza kufa wakiwa na miezi minne. Lakini baada ya chuo kikuu kukabiliana na kiunzi cha kuhuisha wadudu hawa, chuo hicho kingali na kibarua kikubwa zaidi.

 

Na kutokana na hali hiyo, watu wengi wanasema ni afadhali wafe njaa kuliko kuwala wadudu. Hata hivyo,  Profesa Kinyuru na kikundi chake wanasema kuwa wameona watu wengi ambao wamebadili mawazo yao na kuwaelimisha zaidi ya wakulima wapatao 2,000 juu ya suala hilo.

 

Usiku wa kati ya mwezi Novemba na Desemba nchini Uganda huwa ni baraka, kwani huja na chakula chenye rutuba na kitamu.  Senene, huingia eneo la Lyantonde, mji ulioko umbali wa takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Uganda, Kampala.

 

Ambrose Sendagi ni mmoja wa wamiliki wa mitego ya senene, ambapo inapofika usiku wa manane,  huanza harakati za kwenda katika mitego mingine, zaidi ya maili 100 kabla ya jua kuchomoza.

 

 

“Huwa ninaomba Mungu kuwa hali iendelee kama inavyokuwa kabla ya upepo kuwahamisha, kwani huwa wanahamishwa na upepo na mwangaza,” anasema Sendagi na kuendelea kwamba wakati mmoja senene hao walikuwa wakizuiliwa na mwangaza mkali, na hivyo kutumbukia ndani ya mitego wakati ujuzi huo ulipoanza kutumika.

 

Hata hivyo, anasema kuwa wakati mwengine upepo huwa mkali zaidi na  kuharibu mitego. Katika soko la Nakasero, mjini Kampala, wafanyibiashara wana soko kubwa la senene ambapo wengine huwapenda senene hao wanapokuwa na mabawa.

Ieleweka kwamba wadudu hao wanaweza kukaangwa ama kuandaliwa bila mafuta. Nchini humo senene huliwa si kama chakula cha kawaida, kwani wanasayansi wanasema kuwa ni chakula kikamilifu chenye protini.

 

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.