The House of Favourite Newspapers

Wafanyabiashara wafundwa na mjenga uwezo wa kimataifa

0

????????????????????????????????????
Mjenga Uwezo wa Kimataifa wa Masuala ya Kibiashara kutoka Singapore, Harish Babla (kushoto) akimfafanulia jambo Hamza Kasongo (katikati) kabla ya kuanza kwa warsha ya mazungumzo yawapatia uwezo wa kibiashara wafayabiashara hapa nchini iliyoandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya Shrijee’s Traders jana jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwandaaji wa warsha hiyo, Paritosh Babla.

????????????????????????????????????

Paritosh Babla (kushoto) pamoja na Rajesh Bhatia wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shreeji Traders, Vasant Champsi (katikati) ambao ndiyo walikuwa waandaaji na wadhamini wakuu wa warsha ya Masuala ya Kibiashara iliyotolewa kwa wafanyabiashara nchini ya kuwapatia uwezo wa kufanya biashara zao kimataifa hapo jana jijini Dar es Salaam iliyotolewa na Mjenga Uwezo wa Kimataifa wa Masuala hayo toka Singapore, Harish Babla (hayupo pichani)

????????????????????????????????????

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shreeji Traders, Vasant Champsi ambao ndiyo walikuwa waandaaji na wadhamini wakuu wa warsha ya Masuala ya Kibiashara iliyotolewa kwa wafanyabiashara nchini ili kuwapatia uwezo wa kufanya biashara zao kimataifa hapo jana jijini Dar es Salaam iliyotolewa na Mjenga Uwezo wa Kimataifa wa Masuala hayo toka Singapore, Harish Babla (hayupo pichani).

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Baadhi ya wafanyabiashara Nchini wakimsikiliza kwa makini Mjenga Uwezo wa Kimataifa wa Masuala ya Kibiashara kutoka Singapore, Harish Babla wakati wa warsha ya mazungumzo ya kuwapatia mafunzo ya uwezo wa kufanya biashara Kimataifa na Kitaifa kwa ufasaha kwa wafanyabiashara hapa nchini, Warsha hiyo iliandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya Shrijee’s Traders jana jijini Dar es Salaam.

????????????????????????????????????

Mjenga Uwezo wa Kimataifa wa Masuala ya Kibiashara kutoka Singapore, Harish Babla(kushoto)akibadilishana mawazo na Mfanyabiashara Nchini Frank Goyayi baada ya kumalizika kwa warsha ya mazungumzo ya kuwapatia mafunzo ya uwezo wa kibiashara kwa wafanyabiashara hapa nchini ili waweze kufanya biashara zao kwa ufasaha Kimataifa na Kitaifa,Warsha hiyo iliandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya Shrijee’s Traders jana jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, April 2, 2016, Shrijees Traders wamiliki na waendeshaji wa supermarket za Shrijees hapa nchini jana waliandaa mazungumzo ya kibiashara yaliyoongozwa na mjenga uwezo wa kimataifa kutoka nchini Singapore,Harish Babla yalibeba ujumbe “Kuibuka kwa viongozi wapya katika biashara ni kichocheo katika dunia yenye mkanganyiko”

Harish Babla, aliwaongoza washiriki wa mazungumzo hayo ya kutiana moyo ambao ni wafanyabiashara juu ya sifa saba ambazo lazima kiongozi awe nazo ili kuweza kuendelea kuwepo katika dunia yenye mvurugano wa aina mbali mbali. Mazungumzo hayo yaliongezewa uhai na stadi iliyofanywa Chuo kikuu cha Oxford cha Uingereza chini ya Dkt Johari.

Babla alisema, “Dunia imekuwa kama kijiji na hakuna kiongozi katika biashara anaweza kudharau ulimwengu wan je. Zaidi mno, viongozi katika biashara lazima wafikirie mbali zaidi, wawe wenye uthubutu, wabunifu, wenye uelewa wa kutosha juu ya teknalojia na dunia”. Aliongeza Ni muhimu kwa viongozi wa kibiashara katika nchi zinazoendelea kuchukua muda wao wa ziada nje ya kazi kujifunza juu ya mambo mbali mbali,”

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shreeji Traders ambao ndiyo waandaaji na wadhamini wa tukio hilo Vasant Champsi alisema “Wakati makampuni hapa Tanzania yakiendelea kushirikiana na dunia ya nje, ni muhimu kuwa makini kusikiliza mawazo mapya pamoja na sauti zenye uzoefu tofauti ambazo zitasaidia biashara zetu kufanya vizuri ndani ya nchi n ahata nje ya nchi,

Mkurugenzi huyo aliongeza “Shrijees Traders tumeamua kuandaa tukio hili la aina yake hapa Tanzania kwa kumleta mtu mwenye uzoefu na kiongozi mwenye mawazo ya kibiashara ambaye amezaliwa Tanzania na leo amekuja kutushikisha uzoefu na mawazo yake katika masuala ya kibiashara. Tunaamini wafanyabiashara waliohudhuria warsha hii wamenufaika na mafunzo haya na ninapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara na makampuni mengine kuiga mfano na kuwaleta wazungumzaji wengine kwa maendeleo ya nchi yetu,”

Frank Goyayi mmoja ya wafanya biashara wakubwa hapa nchini na mshiriki wa warsha hiyo alisema, “Harish, kupitia njia hii ya kubadilishana mawazo kwa mazungumzo yenye hadithi na mifano, ndani ya dakika 90 tumesafiri duniani kote na kuona umuhimu wa viongozi wapya katika biashara,”

Harish Babla, ni mzaliwa wa Tanzania ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika masuala ya kibiashara na ameshiriki kujengea uwezo makampuni na wafanyabishara wengi duniuani kupitia matukio ya kujifunza
Mwisho.

Leave A Reply