The House of Favourite Newspapers

WAFANYAKAZI CPJ WALIYOSHIKILIWA UHAMIAJI TANZANIA WAACHIWA

Angela Quintal

Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi wa Habari (CPJ) imezitaka Mamlaka nchini Tanzania kuwaachia huru wawakilishi wake wawili barani Afrika, Mratibu wa progamu barani Afrika Angela Quintal na Muthoki Mumo mwakilishi wa CPJ kusini mwa jangwa la Sahara ambao wanadaiwa kukamatwa na Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kuchapishwa kwenye tovuti ya CPJ, afisa mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Idara ya Uhamiaji aliwakamata wafanyakazi hao wawili wa CPJ Angela Quintal na Muthoki Mumo, katika hotelI waliyofikia jijini Dar es Salaam ambapo walikagua vitu walivyokuwa navyo na baadae kuchukua pasiPOSTI zao za kusafiria.

 

Taarifa hiyo inadai wafanyakazi hao ambao wamekuja nchini kwa masuala ya kikazi, inaelezwa kuwa waliondolewa hotelini na kupelekwa sehemu wasioijua ambapo Mkurugenzi mtendaji wa CPJ Joel Simon amesema wana wasiwasi na usalama wa wafanyakazi wao huku wakidai kuwa waliingia Tanzania ki uhalali. Ametoa wito kwa mamlaka nchini Tanzania kuwaachia na kuwarejeshea pasi zao za kusafiria.

 

Muthoki Mumo.

“Ni jambo la kutia wasiwasi mkubwa kuwa huenda simu ya Angela Quintal imetumiwa bila idhini yake. Hatujawasiliana na Angela Quintal au Muthoki Mumo tangu wakamatwe na tunaamini kuwa wote wanazuiliwa na mamlaka za Tanzania,” Joel Simon aliandika kwenye Twitter.

 

Aidha, akizungumza kwa njia ya simu afisa habari wa Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania Ali Mtanda amesema hana habari kuhusiana na taarifa hiyo na kwamba bado hazijafika makao makuu na kutaka kupewa muda, ili kuweza kuthibitisha.

 

Hata hivyo Idara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini imethibitisha kuwa Angela Quintal na Muthoki Mumo wameachiwa huru baada ya kushikiliwa na Maofisa Uhamiaji wa Tanzania Novemba 7.

Comments are closed.