Wafanyakazi Exim Walivyoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja

Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wamefanya matembezi ya amani wakati wa kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024 ambapo wametembea kutoka Makao Makuu ya benki hiyo, Exim Tower mpaka tawi lake la Samora Avenue jijini Dar es Salaam mnamo Oktoba 5, 2024.