The House of Favourite Newspapers

Wafuasi wa Chadema Wakinukisha Mahakamani Kisutu! – Video

 

Wafuasi wa CHADEMA waliofurika katika Mahakama ya Kisutu wamezua sintofahamu baada ya kufanya vurugu wakipiga makelele na kuimba wanataka haki. Hii ni baada ya Jeshi la Polisi kuwazuia kuingia mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano.

 

Wafuasi hao waliokuwa nje ya geti la mahakama hiyo wakiwa wamekusanyika baada ya Jeshi la Polisi kuwazuia kuingia mahakamani kusikiliza kesi ya viongozi hao walianza kupiga makelele wakiimba ‘hatupoi hatupoi, tunataka haki tunataka haki’, hali iliyowalazimu polisi kutia kambi eneo hilo na kuimarisha ulinzi kuhakikisha hakuna uvunjifu wowote wa amani unafanyika.

 

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena leo Machi 29, ili kufanya jitihada za kupata dhamani. Viongozi wengine waandamizi wa Chadema wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni: Vicent Mashinji, John Mnyika, Peter Msigwa, Ester Matiko na Salum Mwalimu, watapandishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa masharti ya dhamana kama ipo au haipo.

KIMENUKA! Wafuasi wa Chadema Mahakamani, Hawapoi, Wanataka Haki!

 

Comments are closed.