JESHI la Polisi limewatimua wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kudaiwa kuanzisha kwa vurugu leo Ijumaa, Novemba 30, 2018.
Hayo yamejiri asubuhi baada ya Polisi kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo wakiwadhibiti wafuasi hao kutokana na kesi kubwa mbili za viongozi wao zinazotarajiwa kutolewa uamuzi leo mahakamani hapo.
Kesi hizo ni iliyofunguliwa na viongozi wa CUF, wakitaka kujua Mwenyekiti wa chama chao, Prof. Ibrahimu Lipumba, ni mwenyekiti halali wa chama hicho au la.
Aidha, kesi ya pili ile ya maombi ya dhamana ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko ambayo inatarajiwa kutolewa uamuzi kuhusu pingamizi lililowasilishwa na upande wa Jamhuri la kutaka rufaa itupwe ya kupinga kufutiwa dhamana kwa washtakiwa hao litupwe kutokana kutofuata vifungu vya kisheria.
Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.
Comments are closed.