The House of Favourite Newspapers

Wafungwa Wahesabiwa Simiyu, RC Ashukuru Ushirikiano na Jeshi la Magereza

0
Dkt. Yahaya Nawanda akiongea na waandishi wa habari

WAKATI Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa katika zoezi la kuhesabu watu na makazi yao (Sensa ya watu na makazi), Jeshi la Magereza mkoani Simiyu wameweza kuhesabu wafungwa kaika magereza ya mkoa huo ambapo wafungwa zaidi ya 100 wamefanikiwa kuhesabiwa.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, DKT. Yahaya Nawanda akiongea baada ya zoezi hiyo alisema:

 

“Wafungwa, Mahabusu Pamoja na Askari wote wanaendelea kuhesabiwa, na tumeshakubalia katika maeneo yetu ya magereza kesho watakuwa wameshamaliza na tutafunga hili zoezi, mpaka sasa hakuna shida yoyote, hakuna tatizo la kimtandao, hakuna tatizo la kiufundi wala aliyeibiwa”

DKT. Yahaya Nawanda amelishukuru Jeshi la Magereza kwa ushirikiano wake katika kufanikisha zoezi hilo

Pia Dkt. Nawanda amelishukuru Jeshi la Magereza kwa ushirikiano mkubwa walio uonesha.

 

Mkaguzi msaidizi wa Magereza, Silvester Malongo amesema zoezi la kuhesabu wafungwa limeenda vizuri na kila kitu kipo sawa.

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply