Wafutiwa shitaka la mauaji baada ya Rais Magufuli kuamuru uchunguzi

MKURUGENZI wa mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, amewafutia shitaka la mauaji watuhumiwa Musa Sadiki na Edward Matiku baada ya agizo la Rais Magufuli la kuchunguzwa kwa kesi hiyo.

 

Rais alitoa agizo hilo baada ya kusoma katika gazeti moja ambapo Musa Sadiki aliandika barua ikionesha alivyobambikiwa kesi ya mauaji na jeshila polisi huku wakichukua fedha taslim Tsh. 788,000 na simu ya mkononi.

 

“Rais alisoma barua hiyo na kunitaka nifuatilie, nimechunguza na nimejiridhisha maelezo ya mtuhumiwa ya gazetini ni ya kweli, yeye na mwenzake nimewafutia mashtaka na ninaagiza warudishiwe mali zao,” alisema Mganga jana.

 

Aidha, DPP aliagiza polisi kuwachunguza waliohusika katika kupanga kesi hiyo namba 8/2018 mkoani Tabora ili wachukuliwe hatua huku akiweka sharti la kutaka kesi zote za jinai zipitie ofisi yake kabla ya kwenda mahakamani.

Toa comment