Wagombea Urais NRA Warejesha Fomu NEC, Wateuliwa – Video
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tikeki ya Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) Janken Kasambala Malik na mgombea mwenza wake, Simai Abdulla wamewasilisha katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, fomu zao za kuomba kuteuliwa kugombea kiti hicho.
Kasambala na Simai wamewasilisha fomu hizo leo Jumanne, Agosti 225, 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC, jijini Dodoma na kupokelewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage.
Jaji Kaijage, kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi amesema wagombea hao wamekidhi vigezo vya kuteuliwa kuwania kiti hicho hivyo Tume imewateua rasmi kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.
TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA