The House of Favourite Newspapers

ads

Wagonjwa wa Corona Kusakwa Nyumba kwa Nyumba

0

KUFUATIA ongezeko la visa na vifo nchini Ufilipino, Polisi pamoja na Mamlaka zitaendesha msako wa nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuwatafuta wagonjwa wa COVID-19 ili kudhibiti maambukizi zaidi.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufilipino, Eduardo Ano amewataka wananchi kuripoti wagonjwa waliopo maeneo yao. Pia, ameonya kuwa wagonjwa ambao watagoma kutoa ushirikiano wanaweza kwenda jela.

 

Akihalalisha oparesheni hiyo, Ano alirejea sheria ya mwaka 2019 kuhusu kuripoti na kufuatilia magonjwa ambapo pia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jonathan Malaya, alisema hatua ya kuwasaka wagonjwa ni ya lazima kwani kuna baadhi ya watu ambao wamekimbia kutoka katika vituo vya matibabu.

 

Ufilipino imerekodi jumla ya visa 57,545 na vifo 1,603 huku wagonjwa waliopona hadi sasa wakifikia 20,459.

 

Source: Reuters

Leave A Reply