The House of Favourite Newspapers

Wagonjwa watekwa, muuguzi anusurika kubakwa

1

charles mkumboNa Joseph Ngilisho, AMANI

ARUSHA: Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Mbuguni wilayani Arumeru jijini hapa, Paulina Mafembo na wagonjwa watano wanadaiwa kutekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka kisha kupelekwa porini kwa nia ya kuwabaka.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni baada ya mtu mmoja kufika katika kituo hicho majira ya saa 10 usiku na kudai kuwa anaumwa na alipofunguliwa ili apatiwe matibabu ndipo watu wengine wanne wakavamia na kuanza kuwapora wajawazito vitu vyao.

Akizungumzia na Amani, Paulina ambaye amenusurika kubakwa alisema baada ya kumfungulia mtu huyo alishangaa kuona wengine wanne wakivamia wakiwa na mapanga na kuanza kuwapokonya wajawazito kila kitu walichokuwa nacho.

“Baada ya hapo walianza kuwabeba wagonjwa ambao ni akina mama na kutokomea nao gizani na kuanza kuwafanyia vitendo vya ubakaji. Na mimi pia nilishikiwa panga na kuamriwa kuvua nguo, nilikubali, yule kibaka alifanya kosa la kuweka panga chini ndipo nikapata mwanya wa kukimbia,” alisema Paulina.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuguni, Wilbard Mungure alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa walishatoa taarifa kwa jeshi la polisi na hatua za kuwasaka watuhumiwa zinaendelea.

Kwa upande wa Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na hakuna mtu anayeshikiliwa kwa tukio hilo.

1 Comment
  1. Billy says

    Hatudanganyiki. Wabakwe wajawazito af wagonjwa wewe ndo ubaki salama? We sema tu ukweli

Leave A Reply