The House of Favourite Newspapers

Wahadhiri Wenye Miaka 65 Waendelee Kufundisha- Dkt Tulia

0

NAIBU Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, ameisisitiza Wizara ya Elimu kuhakikisha wanaliangalia upya suala la Wahadhiri ili waweze kuendelea kufundisha hata baada ya kutimiza miaka 65, kwani wengi wao kwa umri huo ndiyo wanakuwa wamezidi kubobea kwenye taaluma zao.

 

Kauli hiyo ameitoa Bungeni leo Juni 14, 2021, mara baada ya kuibuka mjadala wa Wahadhiri hao kuendelea kufundisha kwa kuwa kuna uhaba mkubwa wa Wahadhiri nchini, swali ambalo liliulizwa na mbunge wa viti maalum Dkt. Thea Ntare, ambapo serikali ilisema kuwa itahakikisha inaangalia namna bora ya kurekebisha sheria hizo ili kuendana na uhitaji wa sasa wa soko la Wahadhiri nchini.

 

Naibu Waziri hili mkalitazame kwa sababu mtu anapofikisha miaka 65 ndiyo amebobea kwenye eneo lake, sasa ukimuondoa huyo ukasema unatengeneza ajira mpya hakuna uhalisia, kwa sababu unayemuajiri haweza kuwa kama huyo mwenye miaka 65, kuna Maprofesa wengine hawana kazi za kufanya lakini wamestaafu na vichwa vyao viko sawa sawa wanaweza kuendelea kufanya kazi,” amesema Dkt. Tulia.

Leave A Reply