The House of Favourite Newspapers

Wahamiaji 81 Wanaswa Dar, Kitakachowakuta ni Hiki! – Video

WIZARA ya Mambo ya Ndani kupitia Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam imewataka wananchi kuwafichua Wahamiaji Haramu wanaoishi kwenye maeneo yao pasipokuwa na vibali maalum vya ukazi ama kufanya shughuli zozote za kibiashara kinyume na sheria.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, SSI – Novaita Mrosso amesema kuwa kuanzia Januari 17, 2019 hadi Januari 29, 2019, Jeshi hilo lilifanya Oparesheni Maalum Katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo walifanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 81 wa makosa mbalimbali ya kiuhamiaji.

 

Mrosso amesema katika uchunguzi waliyofanya kuhusu watuhumiwa hao, wamebaini kati ya watuhumiwa hao 81, raia 30 ni wa kutoka nchi jirani ya burundi na raia wengine wa kigeni wanatoka mataifa mengine ya kigeni na uchunguzi unaendelea dhidi ya uhalali wao wa kuwepo nchini.

 

Aidha, Mrosso amebainisha kuwa watuhumiwa wote waliokwishabainika watachukuliwa hatua  za kisheria zikiwemo kuwafikisha mahakamani na kuwafukuza nchini, na kwamba wanaendelea kuchukua hatua za kuwadhibiti wahamiaji haramu ikiwa ni pamoja na kuendesha zoezi la uhakiki wa taarifa za wageni waliopo kwenye makampuni na taasisi mbalimbali nchini.

 

BREAKING: Uhamiaji Ilivyowanasa Wahamiaji Haramu 81 DSM

Comments are closed.