The House of Favourite Newspapers

Wahamiaji Haramu 53 Kurejeshwa Makwao

0

IDARA ya uhamiaji Mkoa wa katavi inawashikilia jumla ya wahamiaji haramu 58 kutoka nchi ya Afrika Kusini, Burundi na Zambia na kati yao 53 wanatarajia kuondoshwa nchini nakurejeshwa makwao leo Juni 10, 2021.

 

Akitoa taarifa kwa wanahabari Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Katavi Vicent Haule amesema wahamiaji hao haramu wamekamatwa kufuatia Idara ya Uhamiaji kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

 

“Jumla ya wahamiaji 58 wamekamatwa na kuchukuliwa hatua mbalimbali dhidi yao kutokana na makosa, kuna wahamiaji 53 tunawaondosha nchini kuwarudisha kwao Burundi, Congo, miongoni mwao 44 ni rai wa Burundi, DRC wako 7, Zambia 1 na mmoja kutoka Afrika Kusini, hawa tunawaondosha leo” amesema Kamishna Haule

 

Pia Kamishna Haule ameeleza kati ya wahamiaji hao 58, watano wenye makosa ya kujirudia lazima wachunguzwe na kufikishwa Mahakamani ili kujua nani anahusika katika kuwasaidia kuingia nchi kila wakati.

 

“Lakini wengine watano, rai wa Burundi 4 na Rwanda mmoja hawa tunawafikisha Mahakamani kwa sababu wana ile tabia ya kujirudia, unamuondosha leo baada ya mwezi mmoja unakuta wamerudi, tunawapeleka Mahakamani kupunguza network yao ya kuingia bila kufuata utaratibu,”amesema Kamishna Haule.

Leave A Reply