Leo nakuletea orodha ya watu kumi hatari zaidi duniani. Wanatafutwa kutokana na matukio mbalimbali ya kihalifu waliyowahi kuyafanya dhidi ya binadamu na mali zao. Baadhi yao tayari wamekamatwa.
10.AYMAN AL-ZAWAHIRI
Mbabe huyu alikuwa kiongozi wa kundi la Egyptian Islamic Jihad lenye makazi yake jijini Cairo, Misri. Ndiye kiongozi wa juu wa sasa wa kundi hatari la kigaidi la Al-Qaeda.
Uhusiano wake wa karibu na gaidi Osama Bin Laden aliyeuawa mwaka 2012 na majeshi ya Marekani ndiyo ulipelekea achaguliwe kuwa kiongozi wa juu wa kundi hili.
Anatajwa kuhusika na ulipuaji majengo ya Pentagon nchini Marekani na mwaka 2012 alitoa waraka wa kutekwa kwa watalii wote wenye uraia wa nchi za Ulaya wanaotembelea nchi za Kiarabu.
09.OMID TAHVILI
Anashika namba tisa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa zaidi duniani kwa makosa ya uharifu. Ndiye kiongozi wa kundi hatari la uhalifu la Persian Crime Group lenye makazi yake nchini Canada. Mwaka 2007 alifungwa jela na alifanikiwa kutoroka huku akiacha maswali mengi. Anahusishwa na wizi wa pesa na mtandao wa pesa feki nchini Marekani.
08. FELICIAN KABUGA
Mzee huyu anatajwa kuhusika kwenye mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya milioni moja waliuawa. Inasemekana amejificha nchini Kenya na juhudi zote za kumkamata zimeshindikana.
07. JAMES BULGER
Bulger ni mhalifu sugu nchini Marekani akihusishwa na biashara ya madawa ya kulevya na mauaji ya raia wasio na hatia. Anatajwa kuhusika kwenye matukio ya mauaji zaidi ya 19. Anatafutwa na polisi kwa zaidi ya miaka 30 mpaka sasa na anatajwa kuwa na utajiri unaofikia paundi milioni 18.
- ALIMZHAN TOKHATHOUNOV
Mafia huyu raia wa Urusi anatajwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya, utekaji nyara na mauaji ya watu mbalimbali. Anatafutwa na nchi yake na juhudi za kumpata hazijawahi kufanikiwa.
05. JOSEPH KONY
Mpiganaji wa msituni na kiongozi wa kundi la waasi la Lord Resistance Army. Kony raia wa Uganda anayetafutwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa, anatajwa kuhusika kwenye mauaji ya raia wengi wasio na hatia, ubakaji na uporaji. Anatafutwa tangu mwaka 1986.
- SEMION MOGILEVICH
Anafahamika kwa jina la ‘Mhalifu hatari zaidi duniani’, anatajwa kuwa kiongozi mkuu wa kundi la mafia la nchini Urusi linalohusika na mauaji mbalimbali na biashara ya madawa ya kulevya.
03. DAWOOD IBRAHIM
kiongozi mkuu wa Indian Crime Network kundi hili la wahalifu maarufu kwa jina la D-Company linajihusisha na mauaji ya raia, utekaji, ubakaji na biashara ya madawa ya kulevya kwenye nchi za Pakistan, India na Falme za Kiarabu. Anatajwa kama mmoja wa washirika wa karibu wa kundi la Al-Qaeda.
- MATTEO MESSINA DENARO
Anashikiliwa nchini kwake Italia baada ya kutafutwa kwa miaka zaidi ya ishirini, japo amekamatwa ili kujibu tuhuma zinazo mkabili bado anahitajika nchi mbalimbali duniani kwa kuhusishwa na biashara halamu za madawa ya kulevya na utekaji.
Matteo baada ya kukamatwa.
01. JOAQUÍN GUZMÁN
Huyu ndiye mtu hatari zaidi duniani, maarufu kwa jina la El Chappo, kwasasa anashikiliwa nchini kwake Mexico. Mara zote akikamatwa huwa anatoroka, anatajwa kuwa na kikosi hatari kinachojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, huko nchini Marekani wanamtafuta ili wamnyonge.
El Chappo baada ya kukamatwa.
Mbali na uhalifu wake pia ni tajiri anayemiliki kiasi kikubwa cha pesa kutokana na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya. Anahesabika kama mhalifu mwenye nguvu zaidi duniani.
Na Leonard Msigwa/GPL.
Comments are closed.