The House of Favourite Newspapers

WAHENGA’ BADO HAWAJAITWA MAMA

Blandina Changula

KWA sasa mastaa wengi wa Bongo Muvi, wamejaaliwa kupata watoto na kila mmoja anajivunia mtoto wake lakini kuna wengine bado hawajabahatika kupata watoto mpaka leo licha ya kuwa umri wao unawaruhusu.  

 

Kila mmoja ana sababu zake, kuna ambao wanatamani kupata lakini Mungu hajawajaalia, wengine bado hawajapata mtu sahihi lakini wengine wameamua tu kutozaa. Amani linakuletea orodha ya baadhi wasanii ambao umri unawaruhusu lakini bado hawajabahatika kuitwa mama:

 

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’

Ni msanii wa muda mrefu sana tangu kundi la sanaa za maonyesho la Kaole, ambapo mpaka leo hajabahatika kupata mtoto ingawa kuna wakati aliwahi kujinadi kuwa na mtoto lakini uchunguzi zaidi wa Magazeti Pendwa ulibaini hakuwa mwanaye bali alikuwa ni mtoto wa dada yake.

WEMA SEPETU

Watu wengi wanajua kilio chake cha kila siku, anatafuta mtoto lakini mpaka leo hajajaaliwa kupata ingawaje alishawahi kubeba ujauzito wa mshindi wa Big Brother Hot Shot 2014, Idris Sultan lakini ulichoropoka.

MAYASA MRISHO (MAYA)

Ni mmoja wa wasanii wakongwe sana Bongo Muvi lakini mpaka leo na yeye hajabahatika kupata mtoto na mara nyingi hazungumzii hilo wala kuonekana kuwa na shauku na hata hivyo hajawahi kumuweka hadharani mpenzi wake.

RUTH SUKA (MAINDA)

Msanii huyu naye ni mmoja wa wasanii wa zamani waliotokea kundi la Kaole, kipindi cha nyuma alikuwa akitoa kimapenzi na msaa wa vichekesho ambaye sasa hivi ni marehemu, Max lakini baadaye alidaiwa kutoka na muigizaji mwingine, Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpaka sasa hajabahatika kupata mtoto wala kueleza shauku yake ya kupata mtoto.

MARIAM ISMAIL ‘MAMA KUBWA’

Ni kipenzi cha msanii mwenzake Irene Uwoya, japokuwa anaonekana kupenda sana watoto lakini mpaka sasa naye hajabahatika kupata mtoto wala hawajahi kuweka uhusiano wake wa kimapenzi hadharani.

Na. Imelda Mtema

Comments are closed.