The House of Favourite Newspapers

Wahispania Wamfuata Mshambuliaji wa Yanga, Dar Apewa Zawadi

0

JANA asubuhi, mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda, alipata nafasi ya kupokea zawadi ya medali kutoka kwa Lucas Gomez Usoz raia wa Hispania mwenye umri wa miaka nane.

Kijana huyo anayeishi Madrid nchini Hispania, alituma medali hiyo kupitia Ubalozi wa Hispania uliopo Tanzania ambapo Musonda alikabidhiwa na Balozi Jorge Moragas mbele ya Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said.

Usoz, alituma zawadi hiyo kama sehemu ya kuvutiwa na uchezaji wa Musonda baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi akiwa anaitumikia klabu yake ya zamani ya Power Dynamos FC ya nchini Zambia kabla ya kutua Yanga Januari, mwaka huu.

Hafla hii fupi iliyoandaliwa na balozi Jorge, ilifanyika kwenye makazi yake eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vyombo mbalimbali vya habari likiwemo Gazeti la Spoti Xtra.

Akizungumza kwa niaba ya Musonda, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Tumefurahishwa na hiki ambacho kimefanywa kwa mchezaji wetu kwa sababu kitamuongezea thamani mchezaji huyo na ari ya kupambana.

“Kubwa sasa inatakiwa tuwe macho kuona tunamlindaje mchezaji wetu kwa sababu kwa hiki bila shaka macho ya watu wengi yatakuwa kwake zaidi. Lakini ni faraja kwa upande mwingine kuona mchezaji anapata ‘connection’ kubwa.”

STORI NA ISSA LIPONDA

MBETO: ACT – NCCR IMEKULA KWAO, CCM na CHADEMA MNYUKANO MPYA | FRONT PAGE

Leave A Reply