





Zaidi ya wahitimu 90 Chuo Cha Kufundisha Misingi ya Biblia (FBTC Tanzania ) wametakiwa kuwa chachu ya maendeleo katika kuhakikisha wanakwenda kusema ukweli, kufichua maovu, kukemea mapenzi ya kijinsia moja pamoja na kurudisha maadili mema katika jamii.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya Pili ya Chuo Cha kufundisha misingi ya Biblia (FBTC Tanzania ) yaliofanyika katika Kanisa la Pentekoste Assemblies Of God (P.A. G) Mbezi Beach, Katibu Tawala Manispaa ya Kinondoni, Stella Msofe, amesema kuwa viongozi wa dini wanajukumu la kwenda kufundisha maadili ya kitanzania.
Mchungaji wa Kiongozi wa Kanisa la Pentekoste Assemblies Of God (P.A. G) Mbezi Beach, Mchungaji Kiongozi Thomas Dige pamoja na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Chuo Cha FBTC Tanzania, Meshack Mawala, wamesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho, kwani yanakwenda kuleta maisha bora katika jamii, huku wakibainisha kuwa wanaungana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kudumisha amani.
Hata hivyo baadhi ya wahitimu wamesema kuwa wanakwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo kwa lengo la kuisaidia jamii.