The House of Favourite Newspapers

Wahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa kwa Kumuua Dereva Bodaboda

0

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imewahukumu Fred Nyagawa, Isaya Mgimba na James Mteleke kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kumuua kwa kukusudia ndugu Mchape Mkosa.

 

Hukumu hiyo imetolewa jana Ijumaa, Novemba 12, 2021 mahakamani hapo ambapo katika shauri hilo la jinai No. 34/2017 watuhumiwa walitekeleza mauaji hayo Desemba 17, 2015 katika Kijiji cha Mapogolo kilichopo Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

 

Katika hukumu hiyo, Mahakama imesema aliyeuawa (Mchape) alikuwa ni dereva bodaboda ambaye siku ya tukio alikodiwa na walipofika maeneo ya Kijiji cha Mapogolo alinyang’anywa pikipiki kisha kuuawa na wauaji kutoweka na pikipiki hiyo na kwenda kuiuza mkoani Mbeya ambako baadaye ilikamatwa.

 

Mahakama imesema ilidaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa mashamba na ushirikina ambapo Mchape alikuwa akituhumiwa akiwaroga familia ya mshtakiwa wa kwanza na wa nne ambao ndio waliwatafuta washtakiwa wengine wa pili na watatu ili kumuua Mchape kwa malipo ya Tshs. 2,000,000 ambayo walilipwa baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Leave A Reply