The House of Favourite Newspapers

Waigizaji wakubwa, Tuzo za OSCAR wanazisikia kwenye ‘bomba’

0

Will-smith-image3WILL SMITH.

Wakati dunia ikienda kushuhudia ukabidhiwaji wa tuzo za 88 za Oscar zitakazofanyika Februari 16, mwaka huu huko California nchini Marekani, bado macho ya watu wanataka kuona kama mastaa wao wataweza kubeba tuzo hizo kwa mara ya kwanza.

Miongoni mwa vitu ambavyo waigizaji wakubwa wanavitamani ni kunyakua Tuzo za Oscar. Kila muigizaji duniani anatamani kuwa na tuzo hiyo kabatini kwake kwa kuwa ni kubwa, ina heshima kwenye upande wa filamu hata zaidi ya Grammy ambayo hugaiwa kwa watu mbalimbali.

Wapo waigizaji wengi ambao wanaonekana kuwa na mkosi ‘gundu’ wa kutokuipata tuzo hiyo japokuwa wamekuwa waigizaji wakubwa, wenye filamu nzuri na za kuvutia, hebu tuwaone hawa hapa;

Leonardo-DiCaprioLEONARDO DI CAPRIO.

LEONARDO DI CAPRIO
Alianza kujulikana katika Filamu ya Romeo and Juliet, baadaye akaja kuvuma zaidi baada ya kuigiza Filamu ya Titanic na kujulikana kama Jack. Aliendelea kupata mafanikio kwa kuigiza filamu mbalimbali kama Blood Diamond, The Departed na nyingine nyingi, ila pamoja na filamu hizo kali, Tuzo za Oscar zimempitia kushoto kila mwaka. Mwaka huu amechaguliwa kuwania tena na filamu yake ya Revenant kwenye Kipengele cha Picha Bora na Muigizaji Bora, je atafanikiwa? Tusubiri.

JOHNNY DEPP
Ni muigizaji aliyeigiza filamu nyingi tena akiwa na muonekano tofauti. Amevuma kwa filamu kama Pirates Of Caribbean, Lone Ranger, The Tourist na nyingine kibao. Ni miongoni mwa waigizaji wakongwe ila naye tuzo ya Oscar imekuwa ikimpitia kushoto kila mwaka.

ROBERT DOWNEY JR
Staa huyu wa Muvi za Iron Man naye ni miongoni mwa waigizaji wanaolia kukosa tuzo hiyo. Ameigiza filamu nyingi tu ikiwemo Avengers lakini pamoja na umahiri wake huo, hakuwahi kupata tuzo hiyo hata mara moja huku akiwa staa aliyeingiza kiasi kikubwa cha mkwanja.

WILL SMITH
Kama ulifikiri staa huyu aliwahi kubeba Tuzo ya Oscar basi unajidanganya. Amedumu kwenye filamu kwa zaidi ya miaka ishirini, wengi waliamini kwamba angechukua tuzo hiyo alipotoa Muvi ya MIB (Men In Black) mwaka 1997 ila haikuwa hivyo, akakosa na akaendelea kukosa mpaka leo hii anapotamba na Filamu ya Concussion.

HUGH JACKMAN
Muvi zake kali za X Men zilimpa jina, akavuma sana, zikapendwa lakini huwezi kuamini, naye yupo kwenye listi hii ya waigizaji waliokosa tuzo hiyo. Ni kilio chake, anatamani kupata hata moja lakini hilo halikuweza kutokea na kila mwaka amekuwa akiwacheki wenzake wakichukua tu.

bradpittBRAD PITT.

BRAD PITT
Mume wa muigizaji Angeline Jolie ni maarufu sana duniani upande wa filamu lakini pamoja na kuigiza filamu kali kama Mr and Mrs Smith na nyinginezo bado anahangaika kutafuta tuzo hiyo ambayo imekuwa ikichukuliwa hata na waigizaji wachanga. Filamu yake ya The Big Short imechaguliwa kuwania kwenye kipengele cha Picha Bora mwaka huu. Je, ataweza kufuta gundu, tusubiri!

Leave A Reply