The House of Favourite Newspapers

Waimba Injili Walioteswa na Ndoa

0

KWA kawaida, watumishi wa kanisa au watu wanaofuata sana maadili ya dini, huchukuliwa kuwa ndiyo mifano bora katika jamii nyingi duniani. Hawa ni pamoja na Mashehe, Mapadre, Wachungaji, Waimba Injili na wengine wa aina hiyo. Hata hivyo, kibinadamu, baadhi yao hushindwa kuhimili, kuvumilia au kukabiliana na matatizo yanayotokea katika ndoa zao na kujikuta wakiridhia kufarakana, licha ya kuwa huwa tayari wameshaanzisha familia zenye watoto. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya waimba Injili ambao waliteswa na ndoa zao na hatimaye kujikuta wakikaa mbali na wenza wao.

sara1SARA MVUNGI

Mwimbaji huyu wa Injili ambaye amewahi kutamba na nyimbo kama Wewe ni Mungu wangu, Umeniita na nyinginezo, amejaliwa kupata watoto wawili kila mmoja na baba yake, japokuwa amewahi kuingia kwenye ndoa lakini ikavunjika. Hivi karibuni alikiri kwamba aliishi kwenye ndoa kwa miaka 12, lakini hakupata furaha na mpaka sasa anaona kama ana gundu na wanaume, kwani kila anayemtokea kwa gia ya kumuoa, huhitaji tendo la ndoa kwanza, jambo ambalo hukataa na anapowapa sharti kwamba ni mpaka waingie kwenye ndoa, huingia mitini hivyo mpaka sasa hajaolewa tena.
WAIMBAJI 3NEEMA MWAIPOPO

Huyu ni staa wa muziki wa Injili, alitikisa kwa wimbo wake wa Sipati Picha wakati huo akijulikana kwa jina la Neema Mushi kwani alikuwa ameolewa na Mushi ambapo ndoa yao ilivunjika na baadaye kuamua kurudi kwenye jina lake la mwanzo.

Bahatibukuku2BAHATI BUKUKU

Mwanadada huyu ametamba na nyimbo kibao zikiwemo Ikulu ya Mbinguni, Waraka, Mzee Tupatupa na nyingine nyingi. Bahati aliingia kwenye ndoa na Daniel Basila na kujaaliwa kupata watoto wawili wakawa ni bahati mbaya, mwaka 2005 ndoa ilivunjika kutokana na mume kumtuhumu mkewe kutoroshwa nyumbani na mwanaume mwingine, tuhuma ambazo alizikana, akidai kuondoka kutokana na manyanyaso ya mumewe. Mpaka sasa mwanadada huyu hajaolewa tena na anaendelea kumtumikia Mungu.

mbashaaaaFLORA MBASHA NA EMMANUEL MBASHA

Hawa ni waimbaji wa muziki wa Injili ambao walikuwa ni wanandoa na walijaliwa kupata mtoto mmoja. Flora aliachana na mumewe kwa madai kwamba alikuwa akipata manyanyaso makubwa na migogoroya mara kwa mara. Baada ya hapo Emmanuel aliingia kwenye msala mzito wa kudaiwa kumbaka shemeji yake ambapo hukumu ya kesi hiyo ilitoka hivi karibuni katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kuonekana hana hatia. Flora kwa sasa yupo kortini akidai talaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

JANETH MREMA

Staa huyu ameimba nyimbo nyingi ikiwemo Piga Makofi. Aliingia kwenye ndoa na mumewe Jonas Mrema, lakini baadaye kukatokea kutoelewana baina yao kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutoroka na mwanaume mwingine na kwenda kuishi naye kinyumba.

RoseMuhando.jpgROSE MUHANDO

Ni mama wa watoto watatu, kila mmoja na baba yake. Mwanamama huyu ametamba na nyimbo kibao kama Nibebe, Nipe Uvumilivu, Facebook na nyingine nyingi. Rose hajawahi kuolewa ila amezaa tu, ametokea kwenye familia ya kiislam na anamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.

Leave A Reply