The House of Favourite Newspapers

Wajasiriamali Wanawake Wapewa Mafunzo ya Kibiashara

0
Semina ikiendelea
Baadhi ya Viongozi wa NMB wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo(Kushoto) akiteta jambo na Anna Matinde
Wanakwaya wakiimba nyimbo yao.
… Akisoma Hotuba yake mbele ya Mgeni rasmi
Mgeni rasmi, Yusuphu Singo (Katikati) akizundua albamu hiyo.

Wanawake wajasiriamali jijini Dar es Salaam, wamepewa mafunzo maalum ya namna ya kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa mafanikio.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mwika, Sinza jijini hapa ambapo watoa mada mbalimbali, akiwemo Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo na mameneja wa matawi ya benki hiyo, waliwapa mbinu mbalimbali wanawake wajasiriamali, juu ya namna ya kujikwamua kiuchumi.

Wajasiriamali hao, mbali na mambo mengine, wamefundishwa juu ya umuhimu wa kutumia akaunti mpya iliyozinduliwa na benki hiyo, iitwayo Fanikiwa Account, ili kuwa na uhakika wa usalama wa mitaji yao na mikopo ya kibiashara.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Habari, Utamaduni na Sanaa, Yusuph Singo naye alikuwepo kwenye mafunzo hayo ambapo mbali na mambo mengine, amezindua albamu ya muziki wa injili ya Remnant Generation Singers iitwayo ‘Mbiu ya Mgambo Imelia, Sote Tuondoke’ yenye lengo la kuifanya jamii kuwa na maadili na vijana kujitambua.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania, Anna Matinde ambaye  ni mmoja kati ya waandaaji wa mafunzo hayo amesema kuwa ili kuweza kujikwamua kiuchumi  ni vyema kwa wajasiriamali hao kujua umuhimu wa mikopo na mchakato wake.

Nae Meneja wa Kanda wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo, amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa  wadau wa biashara nchini wameona kuwa ni jambo la msingi kuwafahamisha umuhimu wa mikopo ambayo husaidia kukuza kipato na kujijenga kimaisha.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply