Wajerumani Kutafuta Mrithi wa Merkel leo

KINYANG’ANYIRO cha kuamua ni nani atakayemrithi Kansela wa Ujerumani, maarufu na ambaye amehudumu kwa muda mrefu zaidi Angela Merkel kinaweza kuwa kikali huku Wajerumani wakianza uchaguzi wa wabunge leo Septemba 26.

 

Zaidi ya raia milioni 60 wa Ujerumani, leo wanatarajia kushiriki  uchaguzi wa bunge na Ukansela

 

Mgombea wa Ukansela kupitia chama cha SPD Olaf Scholz hivi karibuni alikuwa anaongoza kwenye kura za maoni dhidi ya mgombea wa muungano wa kihafidhina Armin Laschet, kulingana na kura za maoni, Jumla ya vyama 47 na makundi, vinashiriki uchaguzi wa leo.

 

Kansela Angela Merkel, ambaye ameliongoza taifa hilo lenye nguvu zaidi kiuchumi barani Ulaya kwa miaka 16, hagombei katika uchaguzi wa leo.

 


Toa comment