The House of Favourite Newspapers

WAJUE WAREMBO WENYE MIGUU MIKUBWA

Maria Pogrebnyak-Shalatova akiwa amevaa viatu virefu (platform) ambavyo humfanya awe mrefu zaidi na miguu kuonekana mikubwa zaidi.

JARIDA la fasheni la Woman nchini Russia limechapishwa baadhi ya mamodo maarufu nchini humo wanaosemekana wana miguu (makanyagio) mikubwa zaidi duniani, wakiwemo Anastasia Reshetova,  Aiza Anokhima na baadhi ya wake za wanasoka maarufu wa nchini humo.

Reshetova  (21) aliwashangaza mashabiki wake wapatao milioni l.5 kwenye mitandao kwa miguu yake mirefu na mikubwa ikiwa ni pamoja na urefu wa miundi na mapaja yake.

Mrembo mwingine mwenye miguu mikubwa ni Olga Buzova (31) ambaye alikuwa ni mke wa mcheza soka wa timu ya Lokomotiv Moscow, kiungo Dmitri Tarasov (30).  Wawili hao hivi sasa wametalikiana.

 

Kuna mashabiki ambao wamekuwa wakiisifia miguu yake hiyo na wengine kuibeza.

Mrembo Olga Buzova akipozi kuringishia miguu yake mirefu na rangi yake ya maji ya kunde.

Mnyange mwinine wa Russia ambaye amevuta nadhari ya mashabiki kutokana na ukubwa wa miguu yake ni Aiza Anokhina (32) ambaye amebandikwa jina la Victoria Beckham wa Russia.

Victoria ni mke wa aliyekuwa mwanasoka maarufu wa Uingereza, David Beckham.

Licha ya kuwa na umbo dogo kimwili, Anonkhina amekuwa akitania kwamba alibidi awe na miguu midogo pia ili iweze kuendana na mwili huo.

Anastasia Reshetova akionyesha miguu mikubwa yake kwa mashabiki.

Miguu mingine ambayo ni kivutio kwa ukubwa ni ya Maria Pogrebnyak-Shalatova (30), mke wa aliyekuwa mcheza soka wa klabu za Fulham na Reading, mshambuliaji Pavel Pogrebnyak (33) ambaye sasa anachezea klabu ya FC Dynamo Moscow.  Yeye anajulikana kwa kupenda viatu vikubwa na virefu (platform) ambavyo huifanya mikuu yake ionekane mikubwa zaidi na yeye kuonekana mrefu zaidi.

Miguu ya Aiza Anokhina ni miongoni mwa miguu yenye kuvutia kwa ukubwa wake.

Naye Anastasia Volochkova (42) ambaye aliondolewa katika kundi la maonyesho ya michezo, maigizo na nyimbo la Bolshoi Ballet ambalo ni maarufu duniani, amekuwa kivutio kutokana na miguu yake mikubwa.  Volochkova aliondolewa katika kundi hilo kutokana na kuongezeka unene.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA

Comments are closed.