Wakali 40 Jukwaa Moja…Ni Mwendo Wa Singeli Nyerere Day Dar Live

sholo-mwamba-1

Msanii mkali wa Singeli, Sholo Mwamba akiwa Global TV Online kueleza atakavyofanya makamuzi Siku ya Ijumaa ya Oktoba 14 iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Redio Efm ya jijini Dar na Ukumbi wa Dar Live inayotarajiwa kuwa usiku wa kihistoria.

sholo-mwamba-2

Mhariri msadizi wa Gazeti la Amani, Andrew Carlos (kushoto) akiwa na Sholo Mwamba.

sholo-mwamba-3

Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kushoto)  akiwa na Sholo Mwamba katika pozi.

sholo-mwamba-4

Sholo Mwamba (katikati) akiwa na vijana wa Global TV.

Risasi BMM

HII ikufikie wewe mpenzi wa burudani ambaye ulikuwa ukisubiri kwa hamu kuwaona wakali zaidi ya 40 akiwemo mkali wao Msaga Sumu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Ni lini?

Shoo hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Redio Efm ya jijini Dar na Ukumbi wa Dar Live inayotarajiwa kuwa ya kihistoria itafanyika kwa mara ya kwanza ukumbini hapo, Ijumaa ya Oktoba 14, mwaka huu ambayo pia ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julius Nyerere ‘Nyerere Day’.

Akizungumza na Risasi BMM, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, shoo hiyo itatambulika kwa jina la Singeli Michano ambapo historia itaandikwa kwa wakali wa Muziki wa Singeli zaidi ya 40 kukinukisha jukwaa moja mwanzo mwisho.

Huyu hapa Mbizo!

“Itakuwa ni zaidi ya historia kwani haijawahi kutokea nchini wakali wa muziki wa aina moja kupafomu jukwaa moja tena kwa wakati mmoja, hii ndiyo mara ya kwanza tena ndani ya kiwanja kinachoweka historia kila shoo kubwa inapotokea.

 “Unajua tangu muziki huu wa Singeli uanze hatujawahi kuona wanamuziki hawa wakipafomu jukwaa moja ndiyo maana sisi kama Dar Live tumeamua kuwaleta pamoja ili wale wapenzi wa muziki huu wanaousikia tu wapate ladha za tofauti kwa kushuhudia kwa macho yao,” alisema Mbizo.

Wakali watakaopafomu sasa!

Mbizo aliongeza kuwa, mara zote Dar Live imekuwa ikileta vitu vya tofauti ambavyo ni adimu kuvipata katika ukumbi wowote nchini, hivyo katika shoo hii ya Singeli Michano mashabiki watarajie kupata vitu hivyo adimu.

“Tunatarajia hapo baadaye kuwa na orodha ndefu ya wakali zaidi ya 40 watakaopafomu kwenye jukwaa moja lakini hadi sasa ambao tutakuwa nao ni Dogo Niga, Majid Migoma, Dula Makabila, Msaga Sumu, Kaju Mpamba, S Kide, Sholo Mwamba na Segere.

Mtonyo je?

Pamoja na kutaja majina ya baadhi ya wanamuziki watakaopafomu jukwaa moja na kuimba muziki huo wa aina moja, Mbizo pia alisema shoo hiyo itaanza rasmi mida ya saa 8:00 mchana na kuendelea mpaka usiku mnene.

“Huna haja ya kuzichanga sana, ukidumbukiza kibubu cha wiki moja tu ukivunja unapata kiingilio cha Dar Live. Tumeamua kama kuwazawadia mashabiki shoo hii sawa na bure kwani kiingilio kitakuwa kiduchu cha shilingi 5,000 tu kwa kila atakayeingia ukumbini hapo.

“Tunaposema haijawahi kutokea tunamaanisha, vuta picha shoo nzima wakali zaidi ya 40 jukwaa moja kiingilio 5,000 tu uliona wapi kama siyo Dar Live pekee?

“Kikubwa niwaombe tu wapenzi wa burudani hasa wa Muziki wa Singeli kuja kwa wingi ili kuburudika na kuona nani mkali zaidi kwenye muziki huo ambao umeteka soko la muziki kwa sasa na unapendwa na watu wa rika zote, wakiwemo watoto, vijana mpaka wazee,” alisema Mbizo.

Ratiba itakuwaje?

 Akizungumzia ratiba ya siku hiyo, Mbizo alisema kuwa saa 4 asubuhi wasanii wa Singeli watashiriki kwenye zoezi la kupanda miti lililowepewa kauli mbiu ya Mti Wangu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Jackson na viongozi wa Dar Live pamoja na EFM watashiriki.

“Baada ya hapo saa 8 mchana kutakuwa na semina  itakayohusu jinsi ya kuufanya muziki huo kwa kufuata madili lakini pia hadhi za wasanii hao na mambo mengine. Semina hiyo itashirikisha wasanii wa Singeli pamoja na TRA, TCRA, Basata.

“Bila kusahau saa 10 Alasiri kipindi cha Ubaoni kinachorushwa kupitia Redio Efm siku hiyo kitarushwa live kwenye Ukumbi wa Dar live,” alisema Mbizo.


Loading...

Toa comment