The House of Favourite Newspapers

Wakali hawa wakutana kiulaiiini!!

0

Ali Kiba na Victoria Kimani.

KWA kipindi cha hivi karibuni mastaa wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa wakichanua zaidi kimataifa kutokana na muziki huo kukua.Japokuwa wengi wao wameshafanya kolabo na mastaa mbalimbali wa Afrika hususan nchi za Kenya, Nigeria na Sauz lakini kuna mastaa wengine nchini bado hawajafanya na hata wengine kuwa na shauku ya kufanya kolabo na wasanii wa namna hiyo.

Ben Pol na Wangechi.

Hivi karibuni, katika msimu wa tatu wa Coke Studio uliofanyika nchini Kenya, tumeshuhudia mastaa kama Ben Pol, Wangechi, Ali Kiba, Victoria Kimani, Vanessa Mdee na 2 face wakikutana kiulaiiiini na kutengeneza kolabo ambazo zitaanza kusikika Oktoba 10, mwaka huu.

Vee Money na 2 Face (Nigeria)

Vanessa Mdee ‘Vee Money’ anatarajiwa kutinga jukwaa moja na staa kutoka Nigeria, Innocent Ujah Idibia ‘2 Face’ na kukamua nyimbo zao zote kali. Ebu vuta picha 2 Face akiimbishwa Kiswahili ngoma za Vee Money kama vile Me & U na Come Over.

Ben Pol na Wangechi (Kenya)

Staa wa R&B Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ naye atakuwa ni miongoni mwa mastaa aliyekutana kiulaiiini na kufanya kolabo lake na staa kutoka Kenya, Wangechi. Mashabiki watarajie kumsikia Wangechi akiimba na Ben Pol ngoma kama Ningefanyaje, Jikubali pamoja na Sofia.
Ali Kiba na Victoria Kimani (Nigeria)
Patakuwa hapatoshi pale, mkali wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ atakapopanda na staa wa muziki mwenye asili ya Kenya anayefanya shughuli za muziki nchini Nigeria, Victoria Kimani. Hebu vuta picha pale, Kimani anapokamu na Ali Kiba ngoma kama Chekecha Cheketua pamoja na Mwana.

 

Leave A Reply