The House of Favourite Newspapers

Wakali Hawa ‘Wamebuma’ 2017

Msanii wa Bongo Fleva,  Pam D.

MWAKA unazidi kuyoyoma, kwenye upande wa burudani hasa Tasnia ya Muziki, mbali na wanamuziki wenyewe kutathimini nini wamefanya kwa mwaka huu, wadau wa tasnia hiyo hatuwezi kuonekana tumetenda kosa la jinai kupitia nini ambacho wanamuziki wamefanya.

 

Hii inaweza kuwa kidunia, ambapo ukizungumzia wanamuziki waliofanya vizuri hasa kwa Marekani pamoja na wanamuziki wengi, huwezi kuacha kuwataja Taylor Swift na Kendrick Lamar kutokana na albamu zao za Reputation ya Taylor na Damn ya Kendrick kufanya vyema.

Msanii wa Bongo Fleva, Darassa.

Huko ni mbele na hapa Kibongobongo pia listi ipo ndefu, lakini baadhi yao kuna Gigy Money aliyekimbiza na Wimbo wa Papa, Msaga Sumu na Wimbo wa Mwanaume Mashine, pamoja na utitiri wa ngoma za Aslay kama vile Likizo, Pusha na Natamba.

Wapo pia Jux na Wimbo wa Utaniua, Nay wa Mitego na Wapo, Roma na Ngoma ya Zimbabwe na alizoshirikiana na Stamina bila kumsahau Alikiba na Seduce Me yake.

 

Hapo tumezungumzia waliofanya vizuri. Hata hivyo mbali na wanamuziki hao kufanya poa, wapo waliotikisa mwaka jana au miaka michache iliyopita lakini kwa mwaka huu ‘wamebuma’. Hawa hawa baadhi yao;

Msanii wa kike mwenye sauti ya kuvutia Ruby.

Darassa

Mwaka jana Darassa alikuwa gumzo na ngoma ya Muziki, lakini kwa mwaka huu hakuweza kufanya vizuri zaidi na tunaweza kusema amebuma. Ingawa mkali huyu ametoa ngoma kama Utanitoa Roho lakini hakuweza kutoboa kama ilivyokuwa kwa mwaka uliopita.

 

Belle 9

Mkali huyu naye anaingia kwenye listi hii kutokana na kushindwa kutoboa zaidi kimuziki kama ambavyo imekuwa huko nyuma. Belle 9 kwa mwaka huu amejaribu kurudi na Wimbo wa Ma Ole aliofanya na G Nako lakini umebuma na kushindwa kufika mbali.

Msanii wa Bongo Fleva nchini Abelnego Damian, ‘Belle9’.

Navy Kenzo

Tangu watoe Wimbo wa Kamatia, Navy Kenzo wapo kimya. Wimbo uliofanya vizuri kwa mwaka jana katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.

Lakini kwa mwaka huu hawajaachia wimbo wowote ule na Aika nikizungumza naye hivi karibuni alisema waliamua kukaa kimya kwa sababu ya masuala ya uzazi, baada ya yeye kupata ujauzito.

 

Pam D

Mwanadada huyu pia huwezi kukosea kumtia kwenye listi hii naye hajafanya vizuri kwa mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita. Pam D ingawa amejaribu kuja na ngoma kama Daffa na Ngoma Droo aliyomshirikisha Christian Bella lakini bado gemu halikumpokea vizuri sana.

 

Ruby

Nyimbo za Wale Wale na Forever za Rubby zilifanya vizuri mno kwa mwaka jana. Ni ngoma ambazo zilimpa mafanikio makubwa na kumuo-ngezea lundo la mashabiki kutoka kila kona ya nchi na hata nje. Lakini kwa mwaka huu Rubby hajaweza kutoboa kabisa maana hata wimbo wa Kwi Kwi aliomshiri-kisha MC Soudy nao haukufanya poa.

MAKALA NA BONIPHACE NGUMIJE | IJUMAA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.