The House of Favourite Newspapers

WAKALI WA SINGELI, BONGO FLEVA WALIVYOKINUKISHA FUNIKO CONCERT

0
Baraka Daprince.
Mashabiki wakijimwaya.
Country Boy.
Black Rhino kama kawaida yake.
Chibwa akimchezesha shabiki.
Linex akifanya yake.
Man Fongo ‘Hainaga ushemeji’
Pam D naye alinogesha ile mbaya.
Producer T Touch naye alipanda jukwaani kuwaonjesha mashabiki utamu wa biti zake. Yaani ilikuwa si mchezo.

 

Wapenzi wa burudani, Ijumaa iliyopita walishuhudia onesho kali la aina yake lililotambuliwa kama Funiko Cencert lililofanyika kiwanja cha taifa cha burudani cha Dar Live kilichopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

 

Katika tamasha hilo lililoandaliwa na Magic FM kwakushirikiana na Dar Live wasanii kibao walipanda jukwaani kuonesha uwezo wao ambapo umati wa uliofurika ukumbini hapo ulionekana kushindwa kujizua na kuvamia steji kwa mzuka baada ya kunogewa na burudani hiyo.

 

Kila msanii aliyepata nafasi ya kukamua kwenye jukwaa hilo alihakikisha anawanogesha mashabiki wake na kudhihirisha uwepo wake.

 

Miongoni mwa wasanii waliofunika na kuacha historia kwenye onesho hilo ni wakali wa singeli, Man Fongo na Mc Soud ambapo, wakali wa Bongo fleva, Pam D, Moni, Linex, Billnas, Country Boy nao walikamua ile mbaya.

 

Burudani ndani ya ukumbi huo ilikuwa ni bandika bandua huku washereheshaji wa tamasha hilo, Meneja Maneno na T Touch walikuwa wakinogesha kuchombeza na vijinenoneno vya kiburudani.

 

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

 

Leave A Reply