The House of Favourite Newspapers

WAKAMATWA NA MADINI, WAHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA

0
Watuhumiwa wakielekea kusikiliza kesi inayowakabili kabla ya kutolewa hukumu.
Wafanyabiashara watatu ambao ni Mashaka Lucas, Jafarri Hussein na Akifu Mohamed, waliokamatwa na madini ya dhahabu yenye thamani ya Sh. milioni 507.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetoa hukumu kwa wafanyabiashara watatu ambao ni Mashaka Lucas, Jafarri Hussein na Akifu Mohamed, waliokamatwa na madini ya dhahabu yenye thamani ya Sh. milioni 507 waliyokamatwa nayo wakitaka kuyasafirisha bila kibali kwenda nje ya nchi.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa miaka miwili au kulipa faini ya Sh. milioni 9, milioni tatu kila mmoja, baada ya kukutwa na hatia kwa makosa mawili.

Mbali ya hukumu hiyo pia mahakama imeyataifisha madini yao yenye uzito wa kilo 6.242 kuwa mali ya serikali.
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema hukumu hiyo imezingatia kuwa washtakiwa ni wakosaji wa kwanza na walikiri makosa yao.

 

NA DENIS MTIMA/GPL.

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

VIDEO: DK SHIKA KUWEKA HISTORIA USIKU WA 900 ITAPENDEZA

Leave A Reply