The House of Favourite Newspapers

WAKANDARASI DAR WAMUUNGA MKONO MAKONDA KUJENGA MITARO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari. 
Mmoja wa wakandarasi waliojitolea kujenga mitara hiyo raia wa China akizungumza jambo.
..Wakiendelea kuelezea watakavyomuunga mkono Makonda.

ZAIDI ya Kampuni 70 za ukandarasi zimejitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali za jijini Dar es Salaam bure kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda katika kuhakikisha jiji lake linakuwa sehemu safi.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda kufanya ziara katika mkoa wake  na kujionea uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara uliotokana na ukosefu wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi ambao walipokea kwa mikono miwili ombi hilo.

 

Makonda amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuratibu idadi za barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka  kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Mijiji na Vijijini (TARURA)  wilaya kwa ajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro hiyo.

 

Aidha Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea kujenga mitaro hiyo bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilioni ya pesa za serikali.

 

Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vyema kuanzia vifaa na wataalamu kwaajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa.

Comments are closed.