The House of Favourite Newspapers

Wakati Mwingine Kuna Uongo Mtamu Kwenye Mapenzi… Soma Hapa Kujifunza

0

RAFIKI yangu, asante kwa kuendelea kunifuatilia kwenye ukurasa huu; nakuahidi sitakuangusha, nitaendelea kukupa vitu konki hadi uive.

Kwenye mapenzi, mara nyingi mtu anaweza kunufaika kwa maneno ya udanganyifu, lakini mwisho wake, aliyedanganya na aliyedanganywa wanadhurika.

 

Matokeo ya uongo, udanganyifu au hila kwenye mapenzi vina madhara sawa na mtu anayejikuta anatafuna mchanga badala ya ubwabwa.

 

Vijana wengi na hata wazee, wa kike na wa kiume, wamejikuta wanatafuna mchanga au kokoto, badala ya utamu wa mapenzi walioanza nao, wengi wamejeruhiwa na wenzi wao waliojidai wanawapenda, kumbe wana mapenzi ya hila na udanganyifu.

 

Japo kuna wavulana wanaotoswa na mabinti, tena wengine baada ya kuwagharamia hata masomo, lakini asilimia kubwa ya majeruhi ni mabinti.

Wavulana wengi ni wadanganyifu, japo wanaanza kwa mahaba mubashara, wanaishia kujeruhi na kuumiza.

 

Neno la leo, linawaonya vijana wa kiume na mabinti kuwa uongo una madhara kwa wote wawili; japo wavulana wanajiona wana uhuru wa kuharibu na kutafuta wengine.

 

Laana ya udanganyifu inawafuata hadi kwenye ndoa zao, vivyo hivyo kwa wasichana wadanganyifu.

Hata hivyo, kuna wakati ambao yapo mambo mengi sana ambayo ukidanganya hayana madhara katika uhusiano wako, lakini nimekuandalia yale ya muhimu zaidi.

 

Idadi ya wapenzi; nani amewahi kuwa mkweli kwa mpenzi wake mpya kuhusu idadi ya mapatna aliowahi kutoka nao kimapenzi? Hebu anza na wewe mwenyewe?

Jiulize, tangu umeanza mapenzi umetoka faragha na wanaume au wanawake wangapi? Je, upo tayari kumtajia mpenzi wako? Umewahi kufanya hivyo?

 

Rafiki, kati ya mambo ambayo yanaudhi mno kwenye mapenzi ni pale mpenzi anapogundua kwamba mwenzi wake ni jamvi la wageni; yaani ametoka na wapenzi wengi kabla yake.

Wengi wanatamani mno kusikia kwamba wao ni wa pili au wa tatu, vinginevyo akutane na mwanamke ambaye bado hajaanza kabisa mambo ya mapenzi.

 

Rafiki, tuwe wakweli, kumwambia mpenzi wako kwamba umeshatoka kimapenzi na wanaume hamsini, ni sawa na kumtangazia kwamba wewe ni malaya.

Hata kama ni kweli umetoka na idadi hiyo, akikuuliza ipunguze, mwambie yeye ni mwanaume wake wa nne! Wa kwanza alikutoa usichana ukiwa mwanafunzi, baada ya hapo ukaachana naye kabisa na mapenzi yakaisha.

 

Mwingine ulikutana naye chuo, ukamuacha baada ya kugundua kwamba alikuwa akipenda kukutumia tu, wa tatu ulifuma meseji ya mapenzi kwenye simu yake ukaamua kumuacha, yeye ni wa nne!

Mwanaume huyo atajisikia fahari sana kuwa na mwanamke mwenye namba ndogo ya wanaume aliotembea nao, ingawa moyoni mwako unaujua ukweli, lakini inabidi udanganye ili kulinda penzi lako.

 

Uwezo duni faragha; ukiwa na mpenzi wako, si ajabu sana katika mazungumzo yenu ya kawaida, akakuuliza kuhusu uwezo wako wa kucheza gwaride kunako sita kwa sita.

Kwa bahati mbaya kuna rafiki wenye matatizo ya hapa na pale faragha. Baadhi ya wanawake husumbuliwa na tatizo la maumivu wakati wa tendo, kuchelewa kufika mshindo hivyo kuachwa njiani au kupoteza hamu ya tendo.

 

Wanaume wao husumbuliwa na tatizo la kufika mshindo mapema, kushindwa kurudia tendo na kuchoka mapema wakati mwenzake akiwa bado angali anamuhitaji.

Kimsingi matatizo makubwa hapa husababishwa na utayari wa kisaikolojia, maandalizi duni n.k. Unapozungumza na mwenzako kuhusu hili, hutakiwi kumpa taarifa za kweli.

 

Zipo athari kadha wa kadha za kuwa mkweli juu ya matatizo uliyonayo katika eneo hili. Matatizo ya aina hii hutibiwa zaidi na mtu mwenyewe, kugundua udhaifu wake na kuufanyia kazi.

Kama umegundua kwamba unapata maumivu wakati wa tendo, ni wazi kwamba maandalizi si ya kutosha, dawa yake hapo ni kutumia muda mwingi katika maandalizi kabla ya kuanza kazi yenyewe.

 

Kueleza tatizo lako moja kwa moja, kutamfanya mwenzako awe na mawazo, akiamini kwamba ama hutaendana na kasi yake au hatakufurahisha au utamuacha njiani.

Kwa mtazamo huo ni rahisi sana kufikiria kuachana na wewe ili akatafute anayeendana naye.

Kwa leo ninaishia hapa, kwa maoni au ushauri, wasiliana name kwa WhatsApp; 0713 750 910

Leave A Reply