The House of Favourite Newspapers

Wakazi Chanika wachangamkia droo ya ‘Shinda Nyumba’

0

1.Wasomaji wa Gazeti la Championi na Ijumaa wakichangamjkia kununua gazeti hizo kutoka kwa Muuzaji wa Globa,(katikati aliye na flana nyeupe.-001Wasomaji wa Gazeti la Championi na Ijumaa wakichangamkia kununua gazeti hizo kutoka kwa muuzaji wa Global (katikati aliye na fulana nyeupe).2.Wasomaji wa magazeti ya Ijumaa na Championi wa eneo la Chanika Mwisho wakiweka kuponi zao.-001Wasomaji wa Ijumaa na Championi wa eneo la Chanika-Msumbiji wakiweka kuponi zao kwenye ndoo maalum.

3.Msoamaji wa Gazeti la Championi eneo la Kwa Dadi Chanika akielekezwa na Ofisa Usambazaji wa Global, Jordan Ngowi (kulia) namna ya kujaza kuponi yake.-001Msomaji wa Gazeti la Championi wa eneo la Kwa-Dadi Chanika akielekezwa na Ofisa Usambazaji wa Global, Jordan Ngowi (kulia) namna ya kujaza kuponi yake.

4...Ngowi (anayeelekeza katikati) akimwonesha ndoo maalum msomaji wa Gazeti la Championi eneo la Chanika stendi mara baada ya kujaza kuiponi yake.-001 Ngowi (anayeelekeza katikati) akimwonesha ndoo maalum msomaji wa Gazeti la Championi eneo la stendi ya Chanika mara baada ya kujaza kuponi yake.

5.Wasomaji wa magazeti ya Championi na Ijumaa wakiwa wamevalia kofia zilizo na nembo ya Shinda Nyumba.-001Wasomaji wa magazeti ya Championi na Ijumaa wakiwa wamevalia kofia zilizo na nembo ya Shinda Nyumba.

 

WASOMAJI mbalimbali wa magazeti ya Kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi,jana walichangamkia droo ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba huko Chanika nje kidogo ya jijini la Dar kwa kujaza kuponi na kushiriki.

8.Wasoamaji wa Gazeti la Ijumaa na Championi wakiweka kuponi zao ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.-001Maofisa masoko wa Global, Jordan Ngowi na Yohana Mkanda walitembelea maeneo ya Chanika Msumbiji, Masantula, Magenge, Kwa Dadi na Nzasa-Kwa Mwarabu na kugawa zawadi za kofia zenye nembo ya Shinda Nyumba zilizokuwa zikitolewa baada ya kuwakuta wasomaji wakinunua Gazeti la  Ijumaa na Championi.

11.Ofisa Usambazaji,Jordan Ngowi (kulia) akimwelekeza msomaji wa Gazeti la Ijumaa namna ya kujaza kuponi yake.-001Akizungumza na wakazi wa maeneo ya Stendi ya daladala ya Chanika, Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Jordan Ngowi, alisema wasomaji wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kununua magazeti hayo na kukata kuponi ili kujinyakulia zawadi nyingi kwenye droo ya pili ya Shinda Nyumba inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, sambamba na kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi ya nyumba iliyopo eneo la Salasala jijini Dar katika droo ya mwisho.

22.Msomaji wa Gazeti la Ijumaa akijaza kuponi kwenye gari la Matangazo ili kushiriki droo ya pili.-001“Tumekwishatoa zawadi mbalimbali kwa wasomaji wetu kama vile, fulana, kofia, simu za kisasa, runinga na ving’amuzi vya TING katika droo yetu ya kwanza iliyofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.

“Niwasihi wakazi wa Chanika mzidi kununua magazeti yetu ya Global na kujaza kuponi ili muweze kushiriki bahati nasibu yetu. Kitu  muhimu cha kuzingatia ni umri usiopungua zaidi ya miaka 18,” alisema Ngowi.

 Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply