Wakazi Wa Airport, Ukonga Walipongeza Uwazi

WAKAZI mbalimbali wa maeneo ya Air Port na Ukonga-Banana, jijini Dar, leo Jumanne wamekutana uso kwa uso na promosheni ya gazeti la Uwazi inayoongozwa mtu maarufu kwa jina la Mr. Uwazi na kulipongeza gazeti hilo wakisema limesheheni vitu vingi vya kuelimisha na kuburudisha.

Katika promosheni hiyo, Mr. Uwazi alishuhudia wakazi mbalimbali wa maeneo hayo wakichangamkia kulinunua gazeti la Uwazi huku kila mmoja akionesha kuguswa na vitu kama hadithi, machombezo na habari za kipekee zilizomo ndani ya gazeti hilo linalozalishwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd ambao pia wazalishaji wa magazeti mengine bora kama Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi.

“Ni gazeti zuri, tunawapongeza Uwazi wazidi kutuletea vitu vizuri kila siku,” alisema Rose Msekane, mkazi wa Ukonga-Banana.

Mr. Uwazi alisema lengo la  promosheni hiyo ni kuwaweka pamoja wasomaji wake karibu kwa kujua nini kinawavutia.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Msomaji wa Uwazi wa pili kutoka kulia, Raymond Kaje akisoma gazeti la Uwazi akiwa na Mr. Uwazi pamoja rafiki yake.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Ally Shabani akipewa maelekezo ya gazeti la Uwazi na Mr. Uwazi katika eneo la Air Port.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

 Mr. Uwazi akiwa katika picha ya pamoja na msomaji wa gazeti la Uwazi, Mkinga Seif katika eneo la Ukonga Banana.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Rose Msekane akipewa maelekezo kutoka kwa Mr. Uwazi baada ya kununua gazeti la Uwazi katika eneo la Ukonga-Banana

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Mr. Uwazi akisoma gazeti la Uwazi sambamba na msomaji aliyefahamika kwa jina la Supaman Zayumba katika eneo la Ukonga-Banana.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment