UHABA mkubwa wa maji umeyakumba baadhi ya maeneo mkoani Arusha ambapo wananchi wanalazimika kuamka saa tisa usiku na kutembea umbali mrefu kufuata maji kwenye makorongo na visima.
Hali hiyo imemlazimu mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo kufunga safari mpaka kwenye maeneo hayo ambapo amegundua kuwepo kwa madudu mengi, likiwemo la wananchi kuchangishwa fedha kwa ajili ya miradi ambayo haikamiliki.
NA HILALY DAUDI | GLOBAL TV| ARUSHA