The House of Favourite Newspapers

Wakazi Wa Arusha Waomba Kwenye Mnara Wa Saa (Clock Tower) – Video

0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda

Maelfu ya Wakazi wa Mkoa wa Arusha, wamejitokeza kwa wingi kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda kushiriki Matembezi na Maombi ya Kuuombea Mkoa wao na Taifa, ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo Desemba 09, 2024.

Matembezi hayo yameanzia eneo la mzunguko wa Impala kuelekea Mzunguko wa Clock Tower kuelekea Barabara ya Sokoine (Uhuru Road) mpaka mnara wa Mwenge (Azimio la Arusha) ambapo maombi Maalumu yatafanyika.

Kauli Mbiu “Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara; Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yatu”

Maelfu ya Wakazi wa Arusha wakiomba kuzunguka mnara wa saa (clock Tower) ambapo ni eneo la katikati ya bara la Afrika kutoka Kairo – Misri mpaka Afrika ya Kusini.
Maelfu ya Wakazi wa Mkoa wa Arusha, wamejitokeza kwa wingi kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda kushiriki Matembezi na Maombi ya Kuuombea Mkoa wao na Taifa, ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo Desemba 09, 2024.

MAKONDA AONGOZA MAOMBI ARUSHA – NABII MKUU GEORDAVIE – MASHEIKH – MWAMPOSA WABARIKI….

Leave A Reply