The House of Favourite Newspapers

Wakazi wa Arusha Watakiwa Kuwa na Utamaduni wa Kufanya Mazoezi, Kupima Afya Zao

0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mkoani Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa amehimiza wakazi wa mkoa wa Arusha kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza.
Mhe. Mtahengerwa ametoa kauli hiyo mapema leo Jumapili Agosti 4, 2024 mara baada ya kushiriki kwenye mbio za Marathon za Arusha Moyo Marathon 2024 zilizokuwa na lengo la kuchangisha fedha za kusaidia matibabu ya watoto wenye kusumbuliwa na matatizo ya moyo.
Aidha Dkt. Joseph ambaye ni daktari wa Moyo mkoani Arusha amesema serikali inaendelea na ujenzi wa Hospitali kubwa ya moyo mkoani hapa ili kusaidia kupambana na magonjwa ya moyo yayoonekana kushamiri kwenye ukanda wa mikoa ya Kaskazini.
“Hospitali yetu imekuwa na nia thabiti ya kusaidia mkoa na nyanda za juu kaskazini na jitihada zetu kubwa tunakuja kuweka theater ama chumba cha upasuaji wa moyo hapa na ndio dhamira ya mashindano haya na kwasasa tupo kwenye ujenzi wa hospitali yetu kubwa ambayo ina vyumba vitatu vya upasuaji na viwili vya ICU.” Ameongeza Dkt. Joseph.
Kwa upande wao washiriki wa mbio hizo wameshukuru waandaaji wa tukio hilo sambamba na huduma ya vipimo bure waliyoipata mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Leave A Reply