The House of Favourite Newspapers

Dar waendelea kuchangamkia bahati nasibu ya Shinda Nyumba

1

1.Muuzaji wa magazeti ya Global Publishers (katikati) akiwa na msomaji wa gazeti la Uwazi eneo la Tandale sokoni akimwelekeza kujaza kuponi ili kuweza kushriki Bahari Nasibu hiyo.Muuzaji wa magazeti ya Global Publishers (katikati) akiwa na msomaji wa Gazeti la Uwazi eneo la Tandale Sokoni huku akimwelekeza jinsi ya kujaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu hiyo.

2.Msomaji wa Gazeti la Uwazi akishiriki kuweka kuponi yake baada ya kumaliza taratibu za kujaza kuponi iliyo katika gazeti hilo.Msomaji wa Gazeti la Uwazi akiweka kuponi yake baada ya kumaliza kuijaza.

3.Baadhi ya wakazi wa Tandale sokoni wakishudia msomaji wa Gazeti la Uwazi alivyokuwa akijaza kuponi ili kushiriki Bahati Nasibu.Baadhi ya wakazi wa Tandale Sokoni wakishuhudia msomaji wa Gazeti la Uwazi alivyokuwa akijaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu.

4.Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Yohana Mkanda (wapili kushoto) akimwelekeza msomaji wa Gazeti la Uwazi namna ya kujaza kuponi mara baada ya kununua gazeti kwa muuzaji.

Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Yohana Mkanda (wa pili kushoto) akimwelekeza msomaji wa Gazeti la Uwazi namna ya kujaza kuponiĀ  baada ya kununua gazeti hilo.

5.Muuzaji wa Magazeti (aliyevaa kofia) akiwasaidia kujaza kuponi wasomaji wa gazeti la Uwazi ili kuweza kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda na Global.Muuza magazeti (aliyevaa kofia) akiwasaidia kujaza kuponi wasomaji wa Gazeti la Uwazi ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

6...Akiweka kwenye ndoo maalum iliyokuwepo ya bahati nasibu.Msomaji akiweka kuponi kwenye ndoo maalum ya bahati nasibu.

7.Msomaji wa Gazeti la Uwazi mkazi wa eneo la, Magomeni akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati nasibu ya Shinda Nyumba.Msomaji wa Gazeti la Uwazi na mkazi wa eneo la Magomeni (kulia)Ā  akijaza kuponi yake ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

8.Warembo ambao ni wapenzi wa kusoma Gazeti la Uwazi wa eneo Kigogo wajijaza kuponi mara baada ya kununua gazeti kwa muuzaji ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.Warembo ambao ni wapenzi wa kusoma Gazeti la Uwazi wa eneo la Kigogo wakijaza kuponi baada ya kununua gazeti ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

9..Zoezi la kuweka kuponi kwenye ndoo maalum likifanyika.Zoezi la kuweka kuponi kwenye ndoo maalum likifanyika.

10.Mkzi wa eneo la Kigogo akishiriki kujaza kuponi yake mara baada ya kununua gazeti kwa muuzaji wa magazeti ya Global Publishers.Mkazi wa eneo la Kigogo akishiriki kujaza kuponi yake mara baada ya kununua gazeti.

11.Zoezi la kujaza kuponi kwa wakazi wa Kigogo likiendelea. Zoezi la kujaza kuponi kwa wakazi wa Kigogo likiendelea.

ZIKIWA zimepita siku chache baada ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, mapema leo wakazi wa maeneo ya Tandale, Kigogo na Magomeni jijini Dar es Salaam, wameonekana kuchangamkia kununua magazeti ya Global Publishers iliĀ  kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.

Katika bahati nasibu hiyo, msomaji anatakiwa kununua magazeti na kukata kuponi, kisha kuijaza na kuituma kwa njia ya posta au kuifikisha moja kwa moja katika ofisi za Global, Bamaga, Mwenge, Dar au hata kuwafikishia mawakala wa kuuza magazeti waliopo hapa nchini.

Droo ya kwanza ya bahati nasibu hiyo inatarajiwa kuchezeshwa Januari 7, mwaka huu katika viwanja vya Mbagala-Zakhem, Dar,Ā  huku zawadi mbalimbali kama simu za kisasa, dinner sets (vyombo vya ndani) bed sheets, TV, vingā€™amuzi vya TING na pikipiki vitatolewa kwa washindi.
Wafanyakazi wa Global, ndugu zao na watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki.

Stori/ Picha: Denis Mtima/GPL

1 Comment
  1. Global Publishers says

    Tuendelee kuwa pamoja katika shindano hili

Leave A Reply