The House of Favourite Newspapers

Wakili: Makonda Hakupewa Taarifa Kuitwa Mahakamani

0

WAKILI wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Goodchance Reginald amesema mteja wake hakuwa amepewa wito wa kufika mahakamani zaidi ya kuziona habari hizo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

 

Wakili Reginald ameyasema hayo leo katika Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuomba mahakama impe muda zaidi mteja wake ili kuwasilisha hati kinzani dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na mwandishi wa habari, Saed Kubenea, ya kutaka kibali cha kumfungulia kesi ya jinai.

Kufuatia maombi hayo, Hakimu Mkazi, Aron Lyamuya anayesikiliza shauri hilo, amesema mahakama hiyo inampa Makonda siku 21 kuwasilisha hati hizo kinzani dhidi ya maombi ya kumfungulia kesi ya jinai yaliyowasilishwa na Kubenea.

Leave A Reply