The House of Favourite Newspapers

Wakili wa Idris Ashindwa Kufika Mahakamani

0

MSANII na mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultan, ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha kesi namba 60/2020, inayomkabili  na wenzake wawili ya kuchapisha maudhui mtandaoni bila leseni, baada ya wakili wake kushindwa kufika mahakamani.

 

Mbali na Idris Sultan, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Doctor Ulimwengu (28) mkazi wa Mbezi Beach na Isihaka Mwinyimvua (22) ambaye ni msanii na mkazi wa Gongo la Mboto.

 

Idris Sultan ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Luborogwa, ambapo amesema kuwa wakili wake amepata dharura, hivyo hataweza kufika mahakamani hapo.

 

Aidha, Hakimu Luborogwa aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 29.

 

Leave A Reply