WAKILI WA MSIGWA AJITOA KESI YA VIONGOZI CHADEMA

WAKILI anayemtetea Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aitwaye, Jamhuri Johnson, amejitoa kumtetea mteja wake katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wao Freeman Mbowe katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa madai ya kutorishishwa na mwenendo wa kesi hiyo unavyoendeshwa mahakamani hapo.

 

Johnson ametangaza uamuzi huo katika Mahakamani hapo leo Alhamisi, Novemba 8, 2018 mara baada ya upande wa mashtaka kumaliza kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (Ph).

 

 

Akizungumza ndani ya chumba cha mahakama wakili, Jonson ameieleza mahakama kwamba kwa kwa miaka yake zaidi ya 18 ya uwakili hajawahi kuona kesi inaendeshwa kama alivyoiona ya viongozi hao wa Chadema ikiendeshwa.

 

 

Baada ya washtakiwa hao wamesomewa maelezo ya awali huku ya mashtaka yao, waligoma kujibu lolote kutokana na kesi kusomwa upya makosa yao 13 wanayodaiwa kuyatenda, watuhumiwa hao walidai wakili wao hayupo mahakamani hivyo hawawezi kuyakana ama la!.

 

 

Aidha, Mdhamini wa Mbunge Ester Matiko ameieleza Mahakama hiyo kuwa mshtakiwa amepata ziara ya kibunge na yuko nje ya nchi pamoja na kuwasilisha vielelezo ikiwamo tiketi ya ndege aliyoondoka nayo.

 

Kwa upande wake mdhamini wa mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameieleza mahakama kuwa bado yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu na kesi yao imeahirishwa hadi Novemba 12 mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa, Agosti 23 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, wakili Jeremiah Mtobesya aliyekuwa akiwawakilisha Mwenyekiti Mbowe na viongozi wenzake nane wa chama hicho, alijitoa kwenye kesi hiyo.

 

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo  kuhamasisha maandamano Februari 16 mwaka huu siku moja ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni yaliyosababisha mwanafuzni Akwilina kuuawa kwa risasi.

NA DENIS MTIMA | GPL

CHADEMA wafunguka waandishi wa kimataifa waliokamatwa nchini

Toa comment