Wakimbizi wa Ethiopia Wakamatwa Dar, Mmoja Afariki Dunia

WAKIMBIZI kutoka Ethiopia wamekamatwa usiku wa kuamkia jana Jumapili, Aprili 15, 2018 majira ya saa 9.00 usiku wakiwa wamehifadhiwa katika nyumba moja iliyopo Kata ya Goba, jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kwamba polisi walipata taarifa za kuwepo kwa wakimbizi hao baada ya mtu aliyewahifadhi mtaani hapo kwenda kutafuta usafiri wa gari kwa ajili ya kuichukua maiti ya mmoja wao anayesemakana alikufa siku mbili zilizopita ili kwenda kuitupa na ndipo alipobainika.

Aidha, Jeshi la Polisi Dar, bado halijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo, wala haijafahamika walikuwa wanaelekea nchi gani.

CREDIT: JF.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment