WAKINA NORA WAMESEPA NA SANAA YAO

Mwigizaji wa kitambo wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amesema sanaa ya kweli na ya kufurahisha ya maigizo ilikuwa zamani na siyo hii ya sasa. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Nora alisema anakumbuka enzi za Kaole Sanaa ambapo ilikuwa muda ukifika, kila mtu anakimbilia kwenye runinga yake kutazama tamthiliya na kufurahia, lakini utamaduni huo sasa hivi haupo.

“Najivunia kuwajengea watu kupenda sanaa yetu, lakini ukweli ni kwamba sanaa hiyo tulisepa nayo sisi. Sasa hivi imebaki  maonesho tu kwani uhalisia umepotea,” alisema Nora ambaye kwa sasa ameacha uigizaji na kugeukia katika mafundisho ya Dini ya Kiislam


Loading...

Toa comment