WAKIWA KIMAHABA MSITUNI, BABA D, BABY MADAHA LIVE

KAZI na dawa! Baba wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Juma Abdul ‘Baba D’ amenaswa kimahaba msituni na msanii wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ wakati walipokuwa wamekwenda kufanya utafiti wa kazi zao.

 

Tukio hilo ambalo lilipigwa chabo na paparazi wetu limetokea wikiendi iliyopita katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Magamba iliyopo wilayani Lushoto jijini Tanga wakati wawili hao walipokuwa wamekwenda kwenye hifadhi hiyo kutafuta ‘lokesheni’ nzuri za kushutia nyimbo zao mpya.

Wakati wanazungushwa kwenye vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi hiyo iliyo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kuna wakati walijikuta wameachwa peke yao na timu ya maafisa wa msitu huo iliyokuwa ikiwazungusha ndipo walipoutumia mwaya huo kugandana kimahaba.

 

Baada ya paparazi wetu kuwanasa picha za kuwashtukiza wakiwa katika moja ya majengo ya zamani yaliyopo kwenye hifadhi hiyo ambayo ni moja ya vivutio vya kitalii, aliwauliza kama wanafanya hivyo wakiwa ni ‘mtu na mtuwe’, lakini wote wakacheka na kusema hapana!

“Ni kama utani tu si unamjua Baby Madaha mtu wa utani, alipoona wale maafisa hawapo akaanza kunizingua na kunibusubusu, sisi huku tumekuja kuangalia lokesheni kwa kweli tumeoneshwa lokesheni nzuri sana, tutarudi kushuti video zetu kwani Baby ana wimbo mpya na mimi pia,” alisema Baba Diamond.

 

MAUNO YA PAM D NDANI YA STUDIO ZA 255 GLOBAL RADIO


Loading...

Toa comment