The House of Favourite Newspapers

Wakongwe Kazini… Bongo Fleva Kuzaliwa Dar Live

0

nature akiweka mambo sawaJuma Nature

WAKONGWE wa Muziki wa Bongo Fleva wakiongozwa na Dully Sykes, Inspector Haroun, Nature na wengine kibao, Mei 28, mwaka huu wanatarajiwa kuzaliwa upya kwa kugonga shoo ya kihistoria ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

DullyDully Sykes

Akichonga na Risasi Vibes, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mbali na wakali hao, wengine watakaoliteka jukwaa ni Afande Sele, Jafarai, Sister P, Suma G, Abby Skillz na wengineo.

“Siku hiyo, Bongo Fleva itazaliwa upya, hadi makundi yaliyotikisa zamani kama Joint Mob, Zig Zag Crew, Solid Ground Family, Mabaga Fresh, Manzese Crew na mengine yatakuwepo,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 7,000 tu getini.

Leave A Reply