The House of Favourite Newspapers

Wakongwe Walijitutumua, Wapya Wakafanya Kweli 2016

mwana-fa-na-darassaNa Andrew Carlos, Gazeti la Ijumaa, Toleo la Desemba 30, 2016

IKIWA imesalia siku moja kabla ya kumalizika Mwaka wa 2016, katika tasnia ya muziki hususan Bongo Fleva wapo wasanii wapya walioibuka na wengine kuendelea kukubalika kutokana na kutoa nyimbo nzuri.

Lakini pia katika muziki huo wapo wakongwe waliotamba miaka ya nyuma kama Prof. Jay, Jay Moe, TID na wengineo ambao nao hawakuwa nyuma, wamejitutumua mwaka huu na kuendana na kasi ya wasanii wapya walioibuka.

Makala haya yanawachambua baadhi ya wasanii wapya waliofanya na wanaoendelea kufanya kweli sambamba na wakongwe waliojitutumua;

kiba-new

ALI KIBA

Ukipenda muite King Kiba. Mwaka huu aliweza kujitutumua hadi kufikia levo ya kulamba shavu na kampuni kubwa ya kusimamia muziki duniani ya Sony.

Pia Kiba amefanikiwa kukaa levo baada ya kuibuka na Wimbo wa Aje ambao remix yake amem-shirikisha msanii kutoka Nigeria, M.I na kuwa miongoni mwa singo zake za kimataifa kwa mwaka huu.

mwana-fa

MWANA FA

Aliuanza mwaka vizuri kwa kuachia Wimbo wa Asanteni kwa Kuja ambao ulifanya vizuri. Ni miongoni mwa wakongwe wasiochuja katika Muziki wa Bongo Fleva.

Amefunga mwaka vizuri pia kwa Wimbo wa Dume Suruali aliomshirikisha Vee Money ambao unaendelea kutikisa katika chati mbalimbali.

darasaDARASSA

Licha ya miaka ya nyuma kuwahi kutoa nyimbo kama Heya Haye, Weka Ngoma na Sikati Tamaa bado hazikuonesha kudhihirisha kipaji chake. Mwaka huu unaingia moja kwa moja katika vichwa vya mashabiki wa Bongo Fleva na Darassa mwenyewe kuwa ni mwaka usiosahaulika wa mafanikio tangu ameanza muziki.

Nyimbo kama Too Much kisha Muziki alizozitoa mwaka huu zimemfanya kuwa miongoni mwa wasanii wanaoongoza kwa kufanya shoo nyingi Bongo sambamba na kulamba mshiko mzuri.

jide

JIDE

Mwaka huu amejitutumua kweli. Wimbo wa Ndi Ndi Ndi ndiyo umemrudisha kundini na kuwa miongoni mwa wakongwe waliojitutumua.

Wimbo huo umempa mafaniko ya kuingia katika tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Miongoni mwa tuzo anazozishikilia ni Mwanamuziki Bora wa Kike kutoka EATV.

Kwa sasa anabamba na Wimbo wa Sawa na Wao pamoja na Together Remix alioshirikiana na mpenzi wake, Chris ‘Spicy;.

diamond-1DIAMOND

Anaingia katika listi ya walioji-tutumua mwaka huu. Licha ya kuisimamia vema lebo yake ya WCB, Diamond amefanya vizuri. Ameshafanya shoo kubwa nchini Kenya, Zimbabwe, Nigeria na Afrika Kusini.

Moja ya mafanikio yake ya mwaka huu ni kufanya kolabo mbili za kimataifa ambazo ni Marry You akiwa na Ne-Yo pamoja na Kidogo akiwa na P-Square. Pia Wimbo wa Salome umezidi kumjengea heshima katika muziki.

WAPYA WALIOFANYA KWELI

manfongo_0 

MAN FONGO

Licha ya kuimba sana mtaani kwenye vigodoro hakuna aliyekuwa akimjua zaidi. Mwaka huu unabaki kuwa kumbukumbu ya maisha yake na ya Muziki wa Singeli ambao kwa mara ya kwanza umepata shavu kubwa kupigwa katika redio nyingi Bongo.

Wimbo wa Hainaga Ushemeji ni miongoni mwa wimbo wa taifa ambao unapigwa kila sehemu za starehe hususan uswahilini.

BILNAS BILLNAS CHAFU POZI GREGORY ALLSTARTZ DAR MULTITECH ZONEBILLNAS

Baada ya kujitoa katika Lebo ya Radar Entertainment iliyo chini ya msanii TID wengi waliona atapotea kwenye gemu kwani alikuwa na wimbo mmoja tu wa Ligi Ndogo.

Wimbo wa Chafu Pozi uliochezewa mikono na T. Touch ndiyo uliompa heshima na ukomavu kwenye Muziki wa Hip Hop Bongo kwa mwaka huu na kuwa miongoni mwa marapa wanaopendwa kwa sasa.

rayvannyRayvanny

Anasimama kati ya wasanii wapya waliofanya kweli mwaka huu alipoibuka na kuonesha uwezo kupitia Wimbo wa Kwetu kisha Natafuta Kiki.

Kuonesha kuwa hakubahatisha, aliibukia katika Wimbo wa Salome akiwa na Diamond.

harmonize-3Harmonize

Naye ni mmoja wa wasanii wapya wanaounda Lebo ya WCB. Licha ya mwaka jana kufahamika zaidi kupitia Wimbo wa Aiyola na Bado.

Mwaka huu amedhihirisha kuwa anafanya kweli baada ya kuibuka na Wimbo wa Matatizo kisha Inde alioshirikishwa na mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes.

wakali-na-wapya-2016

Gazeti la Ijumaa, Toleo la Desemba 30, 3016

Comments are closed.