Wakurdi waanza oparesheni kukomboa Mji wa Sanjir, Iraq kutoka kwa IS
Wanajeshi wa Kikurdi wakijiandaa kukabiliana na mashambulizi dhidi ya IS
Waumini wa dini ya Yazidi wakikimbia machafuko katika milima ya Sinjar.
Mji wa Sinjar baada ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Wakurdi wakisaidiwa na Marekani.
Hali ilivyokuwa.

Wanajeshi wa Kikurdi.
Milipuko ikitawala katika Mji wa Sinjar.
Sinjar, Iraq
Wanajeshi wa Kikurdi, Kaskazini mwa nchi ya Iraq wameanzisha oparesheni maalum ya kuukomboa Mji wa Sinjar ulioko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Syria kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Islamic State (IS).
Oparesheni hiyo inasaidiwa na muungano unaoongozwa na Jeshi la Marekani wakifanya mashambulio ya anga kwa kutumia ndege zao za kivita.
Mji wa Sinjar ulitekwa na kundi la IS mnamo Agosti, 2014. Maelfu ya waumini wa dini ya Yazidi walikwama baada ya kutorokea Mji wa Sinjar. Mamia ya wanaume waliuawa na wanawake wa Yazidi wakatekwa huku wakitumikishwa kwa ngono.
Shambulio hilo la Sinjar lilikuwa moja ya sababu zilizoifanya Marekani kuanza mashambulizi ya angani kusambaratisha ngome za IS nchini Iraq, baada ya hofu kutanda kuwa, huenda kukatekelezwa mauaji ya halaiki nchini humo. Mwezi uliopita Marekani iliongeza mashambulio yake hadi Syria.
Wachambuzi wa mambo wamesema kuwa, kuukomboa Mji wa Sinjar kutaziba mianya ya mawasiliano kati ya ngome mbili za IS Raqqa na Mosul.

